Quantcast
Channel: CHIMBUKO LETU
Viewing all 911 articles
Browse latest View live

DULLAYO AKIRI MFUMO WA MUZIKI ANAOUFANYA SASA UNAMPOTEZA.

$
0
0


Hitmaker wa Naumia Roho DULLAYO amekiri nyimbo zake kadhaa kumwendea mrama, na anachokifikiria kwa sasa kurejelea mfumo wa awali wa muziki uliomtambulisha.

DULLAYO amesema mfumo aliokuwa akiutumia awali ndio uliokuwa ukimfanya kuheshimika katika Music Industry nakukonga nyoyo za mashabiki.

''Kwa sababu ya matarajio yangu kutofikia mafanikio, kwa hiyo hivi soon nitaachia Video pamoja na audio ikiwa katika miondoko ya Rap, nitaachia mwezi huu inafanana na miondoko ya Naumia Roho so fans wangu wakae mkao wa kumeza kwani watamsikia DULLAYO yuleyule wa kwao wakipindi cha nyuma'' amesema Dullayo.

Kwa upande mwingine DULLAYO kama mzazi amemwelezea Mtoto wake SAMEEL kuwa huenda akaja kuwa mtu maarufu sana kutokana na dalili anazozionesha kupitia vitu anavyovipenda na anampa baraka zote za mafanikio.

''SAMEEL mtoto wangu namlea vizuri, mimi nafikiri mtoto wangu atakuwa star jinsi navyoona utundu wake nini licha ya kuwa ana umri mdogo lakini anapenda sana muziki, japo sipendi mwanangu ajekuwa mwanamuziki napenda asome awe msomi na elimu imkomboe na kuwa msaada mkubwa katika jamii na taifa kwa ujumla'' amesema Dullayo.

NEW VIDEO:- ICE MELODY - SAWA

$
0
0
Ice Melody ni miongoni mwa wasanii wakuangaliwa sana kwa mwaka 2018...... kutokana na uwezo wake mkubwa katika uimbaji.......anakukaribisha kuitazama video yake mpya itwayo SAWA.

MUZIKI SIO KUIMBA, NI UJUMBE WENYE KUKONGA NYOYO ZA MASHABIKI:- SAJNA

$
0
0


Hitmaker wa Sitaki Kuumizwa Sajna amesema kuwa muziki sio kuimba tu ila ni kutengeneza nyimbo ambazo zitakuwa zinadumu kwa kipindi kirefu kuanzia miezi sita na zaidi.

Ujumbe mzito wa mashairi ndio unaomata na wenye kutoa mafunzo ndani ya jamii na sio wenye kusababisha mmomonyoko wa maadili.

 “Hata mama yangu alishaniambia, dada yangu, kaka yangu umeona nyimbo za zamani za akina Mubaraka Mwishehe na mwengineo sio kwamba wamekufa ndio zinafanya vizuri hapana hata leo akisikiliza mtu fulani anapata ujumbe kutokana na kutengeneza wimbo wenye uhalisia" amesema Sajna.

"Huwa wananikumbusha kuwa unaiona Iveta yako ulivyoitengeneza ina uhai, Sitaki kuumizwa, Mganga ni wimbo ambao kila mtu akiusikiliza lazima imkumbushe kitu fulani” ameongeza Sajna.

MR BLUE AWATAJA MBWA KOKO ALIOWALENGA KATIKA NGOMA YAKE.

$
0
0


Rapper na Hitmaker wa Mbwa Koko Mr Blue awataja wahusika waliolengwa katika ngoma yake hiyo, ambayo imefanikiwa kupenya vema kitaani.

Yapo maswali kutoka kwa baadhi ya mashabiki wakijiulizwa amekutwa na jambo gani lililosababisha kuja na ngoma yenye maudhui yakudiss watu?

"Aaaah Mbwa Koko ni kweli wapo na wapo kila kona wapo mbwa wenyewe kabisa,mbwa ambao ni koko wapo binadamu ambao wanafanya mambo kama mbwa koko" amesema Mr Blue

Kupitia The Splash ya Redio Ebony FM, Mr Blue ameenda mbali kwa kutolea mfano baadhi ya watu hao wanaofanya mambo kama Mbwa Koko  wakati akihojiwa na Watangazaji Fredoo Mbunji na Chris Bee.

"Wapo wanawake pia ambao wanafanya mambo kama mbwa koko, wazuri lakini uzuri wao unaishia tu barabarani ukisema umuoe, umchukue au utakiwe umchumbie sio mwanamke wakusema ukae nae na kuna Ma MC pia ambao ni mbwa koko kwa hiyo mbwa koko wapo na hatuwezi kuwakimbia" amehitimisha Mr Blue.

BADO NATEGEMEA MUZIKI KAMA NJIA YA KUJIINGIZIA KIPATO:- RECHO

$
0
0

Mwanamuziki Recho amesema kujitambua kwake ndio njia kuu inayomfanya aendelee kuutegemea muziki zaidi katika kujiingizia kipato cha kuendeshea maisha yake.



''Siri kubwa nikujua ni kitu gani unakifanya, kwa sababu kuna mtu mwingine anakuwa anafanya halafu hajui kitu gani anakifanya, yaani hajielewi yuko wapi? Mimi ninafanya muziki halafu muziki ndio maisha yangu'' amesema Recho



Aidha Recho amesema anategemea sana Muziki umpe mafanikio na jina kubwa ila si kwa skendo. ''Mimi nategemea muziki, unajua skendo iko hivi unaweza ukatoka kwa skendo lakini skendo hiyo hiyo inaweza ikakudondosha vile vile''.



KIPAJI ANAKIDHIHIRISHA VIPI:- Je, humchukua muda gani kuandika ngoma zake?  “Kiukweli nyimbo zangu nyingi huwa siandiki yaani huwa inatokea studio hapo hapo, huwa napenda kuinbgia studio na kuanza kufanya kazi. Muziki ujue ni Mood mtu hawezi akuamsha asubuhi akakuambia uende studio na usifanbye kitu chochote ukiwa hauna mzuka huwezi kufanya kitu''amesema Recho.

ISOME ORODHA YA WASHINDI WA TUZO ZA GRAMMY 2018 ZA NCHINI MAREKANI

$
0
0


Leo alfajiri nchini Marekani kulikuwa na zoezi la ugawaji wa tuzo za Grammy 2018 toleo la 60 ambapo mastaa kibao wakubwa duniani walihudhuria na wengine kushinda tuzo hizo zenye heshima zaidi nchini Marekani.

Wasanii walioibuka na tuzo nyingi usiku wa jana ni Bruno Mars tuzo 6 akifuatiwa na Kendrick Lamar tuzo 5.

Bruno Mars ameshinda kwenye vipengele 6 kikiwemo kipengele cha Album bora ya mwaka ambapo album yake ya ’24k Magic’ imeibuka kidedea ikizipiku album ya 4:44 ya Jay-Z na DAWN ya Kendrick Lamar.
Album of the Year:“Awaken, My Love!” — Childish Gambino4:44 — Jay-ZDAMN. — Kendrick LamarMelodrama — Lorde24K Magic — Bruno Mars — WINNER

Record of the Year:
“Redbone” — Childish Gambino
“Despacito” — Luis Fonsi & Daddy Yankee featuring Justin Bieber
“The Story Of O.J.” — Jay-Z
“HUMBLE.” — Kendrick Lamar
“24K Magic” — Bruno Mars — WINNER

Song of the Year:
“Despacito” — Ramón Ayala, Justin Bieber, Jason “Poo Bear” Boyd, Erika Ender, Luis Fonsi & Marty James Garton, songwriters (Luis Fonsi & Daddy Yankee Featuring Justin Bieber)
“4:44” — Shawn Carter & Dion Wilson, songwriters (Jay-Z)
“Issues” — Benny Blanco, Mikkel Storleer Eriksen, Tor Erik Hermansen, Julia Michaels & Justin Drew Tranter, songwriters (Julia Michaels)
“1-800-273-8255” — Alessia Caracciolo, Sir Robert Bryson Hall II, Arjun Ivatury & Khalid Robinson, songwriters (Logic Featuring Alessia Cara & Khalid)
“That’s What I Like” — Christopher Brody Brown, James Fauntleroy, Philip Lawrence, Bruno Mars, Ray Charles McCullough II, Jeremy Reeves, Ray Romulus & Jonathan Yip, songwriters (Bruno Mars) — WINNER

Best New Artist:Alessia Cara — WINNER
Khalid
Lil Uzi Vert
Julia Michaels
SZA 

Best Pop Solo Performance:
“Love So Soft” — Kelly Clarkson
“Praying” — Kesha
“Million Reasons” — Lady Gaga
“What About Us” — P!nk
“Shape Of You” — Ed Sheeran — WINNER

Best Pop Duo/Group Performance:
“Something Just Like This” — The Chainsmokers & Coldplay
“Despacito” — Luis Fonsi & Daddy Yankee Featuring Justin Bieber
“Thunder” — Imagine Dragons
“Feel It Still” — Portugal. The Man — WINNER
“Stay” — Zedd & Alessia Cara

Best Traditional Pop Vocal Album:Nobody But Me (Deluxe Version) — Michael BubléTriplicate — Bob DylanIn Full Swing — Seth MacFarlaneWonderland — Sarah McLachlanTony Bennett Celebrates 90 — (Various Artists) Dae Bennett, Producer — WINNER

Best Pop Vocal Album:Kaleidoscope EP — ColdplayLust for Life — Lana Del ReyEvolve — Imagine DragonsRainbow — KeshaJoanne — Lady Gaga÷ (Divide) — Ed Sheeran — WINNER

DANCE/ELECTRONIC FIELD 
 Best Dance Recording:
“Bambro Koyo Ganda” — Bonobo Featuring Innov Gnawa
“Cola” — Camelphat & Elderbrook
“Andromeda” — Gorillaz Featuring DRAM
“Tonite” — LCD Soundsystem — WINNER
“Line Of Sight” — Odesza Featuring WYNNE & Mansionair


Best Dance/Electronic Album:Migration — Bonobo3-D The Catalogue — Kraftwerk — WINNERMura Masa — Mura MasaA Moment Apart — OdeszaWhat Now — Sylvan Esso

CONTEMPORARY INSTRUMENTAL FIELD 
 Best Contemporary Instrumental Album:What If — The Jerry Douglas BandSpirit — Alex HanMount Royal — Julian Lage & Chris EldridgePrototype — Jeff Lorber Fusion — WINNERBad Hombre — Antonio Sanchez

ROCK FIELD
 Best Rock Performance:“You Want It Darker” — Leonard Cohen — WINNER
“The Promise” — Chris Cornell
“Run” — Foo Fighters
“No Good” — Kaleo
“Go To War” — Nothing More


Best Metal Performance:
“Invisible Enemy” — August Burns Red
“Black Hoodie” — Body Count
“Forever” — Code Orange
“Sultan’s Curse” — Mastodon — WINNER
“Clockworks” — Meshuggah

Best Rock Song:
“Atlas, Rise!” — James Hetfield & Lars Ulrich, songwriters (Metallica)
“Blood In The Cut” — JT Daly & Kristine Flaherty, songwriters (K.Flay)
“Go To War” — Ben Anderson, Jonny Hawkins, Will Hoffman, Daniel Oliver, David Pramik & Mark Vollelunga, songwriters (Nothing More)
“Run” — Foo Fighters, songwriters (Foo Fighters) — WINNER
“The Stage” — Zachary Baker, Brian Haner, Matthew Sanders, Jonathan Seward & Brooks Wackerman, songwriters (Avenged Sevenfold)

Best Rock Album:Emperor Of Sand — MastodonHardwired…To Self-Destruct — MetallicaThe Stories We Tell Ourselves — Nothing MoreVillains — Queens Of the Stone AgeA Deeper Understanding — The War On Drugs — WINNER

ALTERNATIVE FIELD
 Best Alternative Music Album:Everything Now — Arcade FireHumanz — GorillazAmerican Dream — LCD SoundsystemPure Comedy — Father John MistySleep Well Beast — The National — WINNER

R&B FIELD 
 Best R&B Performance:
“Get You” — Daniel Caesar Featuring Kali Uchis
“Distraction” — Kehlani
“High” — Ledisi
“That’s What I Like” — Bruno Mars — WINNER
“The Weekend” — SZA


Best Traditional R&B Performance:
“Laugh And Move On” — The Baylor Project
“Redbone” — Childish Gambino — WINNER
“What I’m Feelin'” — Anthony Hamilton Featuring The Hamiltones|
“All The Way” — Ledisi
“Still” — Mali Music

Best R&B Song:
“First Began” — PJ Morton, songwriter (PJ Morton)
“Location” — Alfredo Gonzalez, Olatunji Ige, Samuel David Jiminez, Christopher McClenney, Khalid Robinson & Joshua Scruggs, songwriters (Khalid)
“Redbone” — Donald Glover & Ludwig Goransson, songwriters (Childish Gambino)
“Supermodel” — Tyran Donaldson, Terrence Henderson, Greg Landfair Jr., Solana Rowe & Pharrell Williams, songwriters (SZA)
“That’s What I Like” — Christopher Brody Brown, James Fauntleroy, Philip Lawrence, Bruno Mars, Ray Charles McCullough II, Jeremy Reeves, Ray Romulus & Jonathan Yip, songwriters (Bruno Mars) — WINNER

Best Urban Contemporary Album:Free 6LACK — 6LACK“Awaken, My Love!” — Childish GambinoAmerican Teen — KhalidCtrl — SZAStarboy — The Weeknd — WINNER

Best R&B Album:Freudian — Daniel CaesarLet Love Rule — Ledisi24K Magic — Bruno Mars — WINNERGumbo — PJ MortonFeel the Real –Musiq Soulchild

RAP FIELD 
 Best Rap Performance:
“Bounce Back” — Big Sean
“Bodak Yellow” — Cardi B
“4:44” — Jay-Z
“HUMBLE.” — Kendrick Lamar — WINNER
“Bad And Boujee” — Migos Featuring Lil Uzi Vert


Best Rap/Sung Performance:
“PRBLMS” — 6LACK
“Crew” — Goldlink Featuring Brent Faiyaz & Shy Glizzy
“Family Feud” — Jay-Z Featuring Beyoncé
“LOYALTY.” — Kendrick Lamar Featuring Rihanna — WINNER
“Love Galore” — SZA Featuring Travis Scott

Best Rap Song:
“Bodak Yellow” — Dieuson Octave, Klenord Raphael, Shaftizm, Jordan Thorpe, Washpoppin & J White, songwriters (Cardi B)
“Chase Me” — Judah Bauer, Brian Burton, Hector Delgado, Jaime Meline, Antwan Patton, Michael Render, Russell Simins & Jon Spencer,
songwriters (Danger Mouse Featuring Run The Jewels & Big Boi)
“HUMBLE.” — Duckworth, Asheton Hogan & M. Williams II, songwriters (Kendrick Lamar) — WINNER
“Sassy” — Gabouer & M. Evans, songwriters (Rapsody)
“The Story Of O.J.” — Shawn Carter & Dion Wilson, songwriters (Jay-Z)

Best Rap Album:4:44 — Jay-ZDAMN. — Kendrick Lamar — WINNERCulture — MigosLaila’s Wisdom — RapsodyFlower Boy — Tyler, The Creator

COUNTRY FIELD
 Best Country Solo Performance:
“Body Like A Back Road” — Sam Hunt
“Losing You: –Alison Krauss
“Tin Man” — Miranda Lambert
“I Could Use A Love Song” — Maren Morris
“Either Way” — Chris Stapleton — WINNER

Best Country Duo/Group Performance:
“It Ain’t My Fault” — Brothers Osborne
“My Old Man” — Zac Brown Band
“You Look Good” — Lady Antebellum
“Better Man” — Little Big Town — WINNER
“Drinkin’ Problem” — Midland

Best Country Song:
“Better Man” — Taylor Swift, songwriter (Little Big Town)
“Body Like A Back Road” — Zach Crowell, Sam Hunt, Shane McAnally & Josh Osborne, songwriters (Sam Hunt)
“Broken Halos” — Mike Henderson & Chris Stapleton, songwriters (Chris Stapleton) — WINNER
“Drinkin’ Problem” — Jess Carson, Cameron Duddy, Shane McAnally, Josh Osborne & Mark Wystrach, songwriters (Midland)
“Tin Man” — Jack Ingram, Miranda Lambert & Jon Randall, songwriters (Miranda Lambert)

Best Country Album:Cosmic Hallelujah — Kenny ChesneyHeart Break — Lady AntebellumThe Breaker — Little Big TownLife Changes — Thomas RhettFrom a Room: Volume 1 — Chris Stapleton — WINNER

NEW AGE FIELD
 Best New Age Album:Reflection — Brian EnoSongVersation: Medicine — India.ArieDancing On Water — Peter Kater — WINNERSacred Journey Of Ku-Kai, Volume 5 — KitaroSpiral Revelation — Steve Roach

JAZZ FIELD
 Best Improvised Jazz Solo:
“Can’t Remember Why” — Sara Caswell, soloist
“Dance Of Shiva” — Billy Childs, soloist
“Whisper Not” — Fred Hersch, soloist
“Miles Beyond” — John McLaughlin, soloist — WINNER
“Ilimba” — Chris Potter, soloist


Best Jazz Vocal Album:The Journey — The Baylor ProjectA Social Call — Jazzmeia HornBad Ass and Blind — Raul MidónPorter Plays Porter — Randy Porter Trio With Nancy KingDreams and Daggers — Cécile McLorin Salvant — WINNER

Best Jazz Instrumental Album:Uptown, Downtown — Bill Charlap TrioRebirth — Billy Childs — WINNERProject Freedom –Joey DeFrancesco & The PeopleOpen Book — Fred HerschThe Dreamer Is the Dream — Chris Potter

Best Large Jazz Ensemble Album:MONK’estra Vol. 2 — John BeasleyJigsaw — Alan Ferber Big BandBringin’ It — Christian McBride Big Band — WINNERHomecoming — Vince Mendoza & WDR Big Band CologneWhispers on the Wind — Chuck Owen And The Jazz Surge

Best Latin Jazz Album:Hybrido – From Rio To Wayne Shorter — Antonio AdolfoOddara — Jane Bunnett & MaquequeOutra Coisa – The Music Of Moacir Santos — Anat Cohen & Marcello GonçalvesTípico — Miguel ZenónJazz Tango — Pablo Ziegler Trio — WINNER

GOSPEL/ CONTEMPORARY CHRISTIAN MUSIC FIELD
Best Gospel Performance/Song:
“Too Hard Not To” — Tina Campbell
“You Deserve It” — JJ Hairston & Youthful Praise Featuring Bishop Cortez Vaughn
“Better Days” — Le’Andria
“My Life” — The Walls Group
“Never Have To Be Alone” — CeCe Winans — WINNER

Best Contemporary Christian Music Performance/Song:
“Oh My Soul” — Casting Crowns
“Clean” — Natalie Grant
“What A Beautiful Name” — Hillsong Worship — WINNER
“Even If” — MercyMe
“Hills And Valleys” — Tauren Wells

Best Gospel Album:Crossover: Live From Music City — Travis GreeneBigger Than Me — Le’AndriaClose — Marvin SappSunday Song — Anita WilsonLet Them Fall in Love — CeCe Winans — WINNER

Best Contemporary Christian Music Album:Rise — Danny GokeyEchoes (Deluxe Edition) — Matt MaherLifer — MercyMeHills and Valleys — Tauren WellsChain Breaker — Zach Williams — WINNER

Best Roots Gospel Album:The Best Of the Collingsworth Family – Volume 1 — The Collingsworth FamilyGive Me Jesus — Larry CordleResurrection — Joseph HabedankSing It Now: Songs of Faith & Hope — Reba McEntire — WINNERHope for All Nations — Karen Peck & New River

LATIN FIELD 
Best Latin Pop Album:Lo Único Constante — Alex CubaMis Planes Son Amarte — JuanesAmar Y Vivir En Vivo Desde La Ciudad De México, 2017 — La Santa CeciliaMusas (Un Homenaje Al Folclore Latinoamericano En Manos De Los Macorinos) — Natalia LafourcadeEl Dorado — Shakira — WINNER

Best Latin Rock, Urban or Alternative Album:Ayo — Bomba EstéreoPa’ Fuera — C4 Trío & Desorden PúblicoSalvavidas De Hielo — Jorge DrexlerEl Paradise — Los Amigos InvisiblesResidente — Residente — WINNER

Best Regional Mexican Music Album (Including Tejano):Ni Diablo Ni Santo — Julión Álvarez Y Su Norteño BandaAyer Y Hoy — Banda El Recodo De Cruz LizárragaMomentos — Alex CamposArriero Somos Versiones Acústicas — Aida Cuevas — WINNERZapateando En El Norte — Humberto Novoa, producer (Various Artists)

Best Tropical Latin Album:Albita — AlbitaArt of the Arrangement — Doug BeaversSalsa Big Band — Rubén Blades Con Roberto Delgado & Orquesta — WINNERGente Valiente — Silvestre DangondIndestructible — Diego El Cigala

AMERICAN ROOTS MUSIC FIELD
Best American Roots Performance:Killer Diller Blues — Alabama Shakes — WINNER
Let My Mother Live — Blind Boys Of Alabama
Arkansas Farmboy — Glen Campbell
Steer Your Way — Leonard Cohen
I Never Cared For You — Alison Krauss

Best American Roots Song:
“Cumberland Gap” — David Rawlings
“I Wish You Well” — The Mavericks
“If We Were Vampires” — Jason Isbell And The 400 Unit — WINNER
“It Ain’t Over Yet” — Rodney Crowell Featuring Rosanne Cash & John Paul White
“My Only True Friend” –Gregg Allman

Best Americana Album:Southern Blood — Gregg AllmanShine On Rainy Day — Brent CobbBeast Epic — Iron & WineThe Nashville Sound — Jason Isbell And The 400 Unit — WINNERBrand New Day — The Mavericks

Best Bluegrass Album:Fiddler’s Dream — Michael ClevelandLaws Of Gravity — The Infamous Stringdusters — WINNER (TIE)Original — Bobby OsborneUniversal Favorite — Noam PikelnyAll The Rage – In Concert Volume One [Live] — Rhonda Vincent And The Rage — WINNER (TIE

Best Traditional Blues Album:Migration Blues — Eric BibbElvin Bishop’s Big Fun Trio — Elvin Bishop’s Big Fun TrioRoll And Tumble — R.L. BoyceSonny & Brownie’s Last Train — Guy Davis & Fabrizio PoggiBlue & Lonesome — The Rolling Stones — WINNER

Best Contemporary Blues Album:Robert Cray & Hi Rhythm — Robert Cray & Hi RhythmRecorded Live In Lafayette — Sonny LandrethTajMo — Taj Mahal and Keb’ Mo’ — WINNERGot Soul — Robert Randolph & The Family BandLive From The Fox Oakland — Tedeschi Trucks Band

Best Folk Album:Mental Illness — Aimee Mann — WINNERSemper Femina — Laura MarlingThe Queen Of Hearts — Offa RexYou Don’t Own Me Anymore — The Secret SistersThe Laughing Apple — Yusuf / Cat Stevens

Best Regional Roots Music Album:Top Of the Mountain — Dwayne Dopsie And The Zydeco HellraisersHo’okena 3.0 — Ho’okenaKalenda — Lost Bayou Ramblers — WINNERMiyo Kekisepa, Make A Stand [Live] — Northern CreePua Kiele — Josh Tatofi

REGGAE FIELD 
Best Reggae Album:Chronology — ChronixxLost In Paradise — Common KingsWash House Ting — J BoogStony Hill — Damian “Jr. Gong” Marley — WINNERAvrakedabra — Morgan Heritage

Best World Music Album:Memoria De Los Sentidos — Vicente AmigoPara Mi — BuikaRosa Dos Ventos — Anat Cohen & Trio BrasileiroShaka Zulu Revisited: 30th Anniversary Celebration — Ladysmith Black Mambazo — WINNERElwan — Tinariwen

Best Children’s Album:Brighter Side — Gustafer YellowgoldFeel What U Feel — Lisa Loeb — WINNERLemonade — Justin RobertsRise Shine #Woke — Alphabet RockersSongs Of Peace & Love For Kids & Parents Around The World — Ladysmith Black Mambazo

Best Spoken Word Album (Includes Poetry, Audio Books & Storytelling):Astrophysics For People In A Hurry — Neil Degrasse TysonBorn To Run — Bruce SpringsteenConfessions Of A Serial Songwriter — Shelly PeikenOur Revolution: A Future to Believe In (Bernie Sanders) — Bernie Sanders And Mark RuffaloThe Princess Diarist — Carrie Fisher — WINNER

Best Comedy Album:The Age Of Spin & Deep In The Heart Of Texas — Dave Chappelle — WINNERCinco — Jim GaffiganJerry Before Seinfeld — Jerry SeinfeldA Speck Of Dust — Sarah SilvermanWhat Now? — Kevin Hart

Best Musical Theater Album:Come From Away — Ian Eisendrath, August Eriksmoen, David Hein, David Lai & Irene Sankoff, producers; David Hein & Irene Sankoff, composers/lyricists (Original Broadway Cast Recording)Dear Evan Hansen — Ben Platt, principal soloist; Alex Lacamoire, Stacey Mindich, Benj Pasek & Justin Paul, producers; Benj Pasek & Justin Paul, composers/lyricists (Original Broadway Cast Recording) — WINNERHello, Dolly! — Bette Midler, principal soloist; Steven Epstein, producer (Jerry Herman, composer & lyricist) (New Broadway Cast Recording) 

Best Compilation Soundtrack For Visual Media:Baby Driver — (Various Artists)Guardians Of the Galaxy Vol. 2: Awesome Mix Vol. 2 — (Various Artists)Hidden Figures: The Album — (Various Artists)La La Land — (Various Artists) — WINNERMoana: The Songs — (Various Artists)

Best Score Soundtrack For Visual Media:Arrival — Jóhann Jóhannsson, composerDunkirk — Hans Zimmer, composerGame Of Thrones: Season 7 — Ramin Djawadi, composerHidden Figures — Benjamin Wallfisch, Pharrell Williams & Hans Zimmer, composersLa La Land — Justin Hurwitz, composer — WINNER

Best Song Written For Visual Media:
“City Of Stars” — Justin Hurwitz, Benj Pasek & Justin Paul, songwriters (Ryan Gosling & Emma Stone)
“How Far I’ll Go” — Lin-Manuel Miranda, songwriter (Auli’i Cravalho) — WINNER
“I Don’t Wanna Live Forever (‘Fifty Shades Darker’)” — Jack Antonoff, Sam Dew & Taylor Swift, songwriters (Zayn & Taylor Swift)
“Never Give Up” — Sia Furler & Greg Kurstin, songwriters (Sia)
“Stand Up For Something” — Common & Diane Warren, songwriters (Andra Day Featuring Common

Best Instrumental Composition:
“Alkaline” — Pascal Le Boeuf, composer (Le Boeuf Brothers & JACK Quartet)
“Choros #3” — Vince Mendoza, composer (Vince Mendoza & WDR Big Band Cologne)
“Home Free (For Peter Joe)” — Nate Smith, composer (Nate Smith)
“Three Revolutions” — Arturo O’Farrill, composer (Arturo O’Farrill & Chucho Valdés) — WINNER
“Warped Cowboy” — Chuck Owen, composer (Chuck Owen And The Jazz Surge)

Best Arrangement, Instrumental or A Cappella:
“All Hat, No Saddle” — Chuck Owen, arranger (Chuck Owen And The Jazz Surge)
“Escapades For Alto Saxophone And Orchestra From Catch Me If You Can” — John Williams, arranger (John Williams) — WINNER
“Home Free (For Peter Joe)” — Nate Smith, arranger (Nate Smith)
“Ugly Beauty/Pannonica” — John Beasley, arranger (John Beasley)
“White Christmas” — Chris Walden, arranger (Herb Alpert)

Best Arrangement, Instruments and Vocals:
“Another Day Of Sun” — Justin Hurwitz, arranger (La La Land Cast)
“Every Time We Say Goodbye” — Jorge Calandrelli, arranger (Clint Holmes Featuring Jane Monheit)
“I Like Myself” — Joel McNeely, arranger (Seth MacFarlane)
“I Loves You Porgy/There’s A Boat That’s Leavin’ Soon For New York” — Shelly Berg, Gregg Field, Gordon Goodwin & Clint Holmes, arrangers (Clint Holmes Featuring Dee Dee Bridgewater And The Count Basie Orchestra)
“Putin” — Randy Newman, arranger (Randy Newman) — WINNER 

Best Recording Package:El Orisha De La Rosa — Claudio Roncoli & Cactus Taller, art directors (Magín Díaz) — WINNER (TIE)Mura Masa — Alex Crossan & Matt De Jong, art directors (Mura Masa)Pure Comedy (Deluxe Edition) — Sasha Barr, Ed Steed & Josh Tillman, art directors (Father John Misty) — WINNER (TIE)Sleep Well Beast — Elyanna Blaser-Gould, Luke Hayman & Andrea Trabucco-Campos, art directors (The National)Solid State — Gail Marowitz, art director (Jonathan Coulton)

Best Boxed Or Special Limited Edition Package:Bobo Yeye: Belle Epoque In Upper Volta — Tim Breen, art director (Various Artists)Lovely Creatures: The Best Of Nick Cave And The Bad Seeds (1984 – 2014) — Tom Hingston, art director (Nick Cave And The Bad Seeds)May 1977: Get Shown The Light — Masaki Koike, art director (Grateful Dead)The Voyager Golden Record: 40th Anniversary Edition — Lawrence Azerrad, Timothy Daly & David Pescovitz, art directors (Various Artists) — WINNERWarfaring Strangers: Acid Nightmares — Tim Breen, Benjamin Marra & Ken Shipley, art directors (Various Artists) 

Best Album Notes:Arthur Q. Smith: The Trouble With The Truth — Wayne Bledsoe & Bradley Reeves, album notes writers (Various Artists)Big Bend Killing: The Appalachian Ballad Tradition — Ted Olson, album notes writer (Various Artists)The Complete Piano Works Of Scott Joplin — Bryan S. Wright, album notes writer (Richard Dowling)Edouard-Léon Scott De Martinville, Inventor Of Sound Recording: A Bicentennial Tribute— David Giovannoni, album notes writer (Various Artists)Live At The Whisky A Go Go: The Complete Recordings — Lynell George, album notes writer (Otis Redding) — WINNERWashington Phillips And His Manzarene Dreams — Michael Corcoran, album notes writer (Washington Phillips) 

Best Historical Album:Bobo Yeye: Belle Epoque In Upper Volta — Jon Kirby, Florent Mazzoleni, Rob Sevier & Ken Shipley, compilation producers; Jeff Lipton & Maria Rice, mastering engineers (Various Artists)The Goldberg Variations – The Complete Unreleased Recording Sessions June 1955 — Robert Russ, compilation producer; Matthias Erb, Martin Kistner & Andreas K. Meyer, mastering engineers (Glenn Gould)Leonard Bernstein – The Composer — Robert Russ, compilation producer; Martin Kistner & Andreas K. Meyer, mastering engineers (Leonard Bernstein)Sweet As Broken Dates: Lost Somali Tapes From The Horn Of Africa — Nicolas Sheikholeslami & Vik Sohonie, compilation producers; Michael Graves, mastering engineer (Various Artists)Washington Phillips And His Manzarene Dreams — Michael Corcoran, April G. Ledbetter & Steven Lance Ledbetter, compilation producers; Michael Graves, mastering engineer (Washington Phillips)

PRODUCTION, NON-CLASSICAL FIELD 
Best Engineered Album, Non-Classical:Every Where Is Some Where — Brent Arrowood, Miles Comaskey, JT Daly, Tommy English, Kristine Flaherty, Adam Hawkins, Chad Howat & Tony Maserati, engineers; Joe LaPorta, mastering engineer (K.Flay)Is This The Life We Really Want? — Nigel Godrich, Sam Petts-Davies & Darrell Thorp, engineers; Bob Ludwig, mastering engineer (Roger Waters)Natural Conclusion — Ryan Freeland, engineer; Joao Carvalho, mastering engineer (Rose Cousins)No Shape — Shawn Everett & Joseph Lorge, engineers; Patricia Sullivan, mastering engineer (Perfume Genius)24K Magic — Serban Ghenea, John Hanes & Charles Moniz, engineers; Tom Coyne, mastering engineer (Bruno Mars) — WINNER
Producer Of the Year, Non-Classical:
Calvin Harris
Greg Kurstin — WINNER
Blake Mills
No I.D.
The Stereotypes

Best Remixed Recording:
“Can’t Let You Go (Louie Vega Roots Mix)” — Louie Vega, remixer (Loleatta Holloway)
“Funk O’ De Funk (SMLE Remix)” — SMLE, remixers (Bobby Rush)
“Undercover (Adventure Club Remix)” — Leighton James & Christian Srigley, remixers (Kehlani)
“A Violent Noise (Four Tet Remix)” — Four Tet, remixer (The xx)
“You Move (Latroit Remix)” — Dennis White, remixer (Depeche Mode) — WINNER

Best Surround Sound Album:Early Americans — Jim Anderson, surround mix engineer; Darcy Proper, surround mastering engineer; Jim Anderson & Jane Ira Bloom, surround producers (Jane Ira Bloom) — WINNERKleiberg: Mass For Modern Man — Morten Lindberg, surround mix engineer; Morten Lindberg, surround mastering engineer; Morten Lindberg, surround producer (Eivind Gullberg Jensen & Trondheim Symphony Orchestra And Choir)So Is My Love — Morten Lindberg, surround mix engineer; Morten Lindberg, surround mastering engineer; Morten Lindberg, surround producer (Nina T. Karlsen & Ensemble 96)3-D The Catalogue — Fritz Hilpert, surround mix engineer; Tom Ammermann, surround mastering engineer; Fritz Hilpert, surround producer (Kraftwerk)Tyberg: Masses — Jesse Brayman, surround mix engineer; Jesse Brayman, surround mastering engineer; Blanton Alspaugh, surround producer (Brian A. Schmidt, Christopher Jacobson & South Dakota Chorale)

Best Engineered Album, Classical:Danielpour: Songs Of Solitude & War Songs — Gary Call, engineer (Thomas Hampson, Giancarlo Guerrero & Nashville Symphony)Kleiberg: Mass For Modern Man — Morten Lindberg, engineer (Eivind Gullberg Jensen, Trondheim Vokalensemble & Trondheim Symphony Orchestra)
Schoenberg, Adam: American Symphony; Finding Rothko; Picture Studies — Keith O. Johnson & Sean Royce Martin, engineers (Michael Stern & Kansas City Symphony)
Shostakovich: Symphony No. 5; Barber: Adagio — Mark Donahue, engineer (Manfred Honeck & Pittsburgh Symphony Orchestra) — WINNERTyberg: Masses — John Newton, engineer; Jesse Brayman, mastering engineer (Brian A. Schmidt, Christopher Jacobson & South Dakota Chorale)

Producer Of the Year, Classical:
Blanton Alspaugh
Manfred Eicher
David Frost — WINNER
Morten Lindberg
Judith Sherman 

Best Orchestral Performance:
Concertos For Orchestra — Louis Langrée, conductor (Cincinnati Symphony Orchestra)
Copland: Symphony No. 3; Three Latin American Sketches — Leonard Slatkin, conductor (Detroit Symphony Orchestra)
Debussy: Images; Jeux & La Plus Que Lente — Michael Tilson Thomas, conductor (San Francisco Symphony)
Mahler: Symphony No. 5 — Osmo Vänskä, conductor (Minnesota Orchestra)
Shostakovich: Symphony No. 5; Barber: Adagio — Manfred Honeck, conductor (Pittsburgh Symphony Orchestra) — WINNER

Best Opera Recording:
Berg: Lulu — Lothar Koenigs, conductor; Daniel Brenna, Marlis Petersen & Johan Reuter; Jay David Saks, producer (The Metropolitan Opera Orchestra)
Berg: Wozzeck — Hans Graf, conductor; Anne Schwanewilms & Roman Trekel; Hans Graf, producer (Houston Symphony; Chorus Of Students And Alumni, Shepherd School Of Music, Rice University & Houston Grand Opera Children’s Chorus) — WINNER
Bizet: Les Pêcheurs De Perles — Gianandrea Noseda, conductor; Diana Damrau, Mariusz Kwiecień, Matthew Polenzani & Nicolas Testé; Jay David Saks, producer (The Metropolitan Opera Orchestra; The Metropolitan Opera Chorus)
Handel: Ottone — George Petrou, conductor; Max Emanuel Cencic & Lauren Snouffer; Jacob Händel, producer (Il Pomo D’Oro)
Rimsky-Korsakov: The Golden Cockerel — Valery Gergiev, conductor; Vladimir Feliauer, Aida Garifullina & Kira Loginova; Ilya Petrov, producer (Mariinsky Orchestra; Mariinsky Chorus)

Best Choral Performance:Bryars: The Fifth Century — Donald Nally, conductor (PRISM Quartet; The Crossing) — WINNER
Handel: Messiah — Andrew Davis, conductor; Noel Edison, chorus master (Elizabeth DeShong, John Relyea, Andrew Staples & Erin Wall; Toronto Symphony Orchestra; Toronto Mendelssohn Choir)
Mansurian: Requiem — Alexander Liebreich, conductor; Florian Helgath, chorus master (Anja Petersen & Andrew Redmond; Münchener Kammerorchester; RIAS Kammerchor)
Music Of the Spheres — Nigel Short, conductor (Tenebrae)
Tyberg: Masses — Brian A. Schmidt, conductor (Christopher Jacobson; South Dakota Chorale)

Best Chamber Music/Small Ensemble Performance:
Buxtehude: Trio Sonatas, Op. 1 — Arcangelo
Death & The Maiden — Patricia Kopatchinskaja & The Saint Paul Chamber Orchestra — WINNER
Divine Theatre – Sacred Motets By Giaches De Wert — Stile Antico
Franck, Kurtág, Previn & Schumann — Joyce Yang & Augustin Hadelich
Martha Argerich & Friends – Live From Lugano 2016 — Martha Argerich & Various Artists

Best Classical Instrumental Solo:
Bach: The French Suites — Murray Perahia
Haydn: Cello Concertos — Steven Isserlis; Florian Donderer, conductor (The Deutsch Kammerphilharmonie Bremen)
Levina: The Piano Concertos — Maria Lettberg; Ariane Matiakh, conductor (Rundfunk-Sinfonieorchester Berlin)
Shostakovich: Violin Concertos Nos. 1 & 2 — Frank Peter Zimmermann; Alan Gilbert, conductor (NDR Elbphilharmonie Orchester)
Transcendental — Daniil Trifonov — WINNER

Best Classical Solo Vocal Album:
Bach & Telemann: Sacred Cantatas — Philippe Jaroussky; Petra Müllejans, conductor (Ann-Kathrin Brüggemann & Juan de la Rubia; Freiburger Barockorchester)
Crazy Girl Crazy – Music By Gershwin, Berg & Berio — Barbara Hannigan (Orchestra Ludwig) — WINNER
Gods & Monsters — Nicholas Phan; Myra Huang, accompanist
In War & Peace – Harmony Through Music — Joyce DiDonato; Maxim Emelyanychev, conductor (Il Pomo D’Oro)
Sviridov: Russia Cast Adrift — Dmitri Hvorostovsky; Constantine Orbelian, conductor (St. Petersburg State Symphony Orchestra & Style Of Five Ensemble)

Best Classical Compendium:
Barbara — Alexandre Tharaud; Cécile Lenoir, producer
Higdon: All Things Majestic, Viola Concerto & Oboe Concerto — Giancarlo Guerrero, conductor; Tim Handley, producer — WINNER
Kurtág: Complete Works For Ensemble & Choir — Reinbert de Leeuw, conductor; Guido Tichelman, producer
Les Routes De L’Esclavage — Jordi Savall, conductor; Benjamin Bleton, producer
Mademoiselle: Première Audience – Unknown Music Of Nadia Boulanger — Lucy Mauro; Lucy Mauro, producer

Best Contemporary Classical Composition:
Danielpour: Songs Of Solitude — Richard Danielpour, composer (Thomas Hampson, Giancarlo Guerrero & Nashville Symphony)
Higdon: Viola Concerto — Jennifer Higdon, composer (Roberto Díaz, Giancarlo Guerrero & Nashville Symphony) — WINNER
Mansurian: Requiem — Tigran Mansurian, composer (Alexander Liebreich, Florian Helgath, RIAS Kammerchor & Münchener Kammerorchester)
Schoenberg, Adam: Picture Studies — Adam Schoenberg, composer (Michael Stern & Kansas City Symphony)
Zhou Tian: Concerto For Orchestra — Zhou Tian, composer (Louis Langrée & Cincinnati Symphony Orchestra) 

Best Music Video:
“Up All Night” — Beck
“Makeba” — Jain
“The Story Of O.J.” — Jay-Z
“Humble.” — Kendrick Lamar — WINNER
“1-800-273-8255” — Logic Featuring Alessia Cara & Khalid

Best Music Film:One More Time With Feeling — Nick Cave & The Bad SeedsLong Strange Trip — (The Grateful Dead)The Defiant Ones — (Various Artists) — WINNERSoundbreaking — (Various Artists)Two Trains Runnin’ — (Various Artists)

NEW VIDEO:- MBOSSO - WATAKUBALI

PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG KUTUA ARSENAL FC

$
0
0


Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji matata kutoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund kwa karibu £60m.

Lakini uhamisho huo hautaidhinishwa hadi pale Dortmund watakapopata mchezaji wa kujaza pengo ambalo litaachwa na Aubameyang.

Taarifa zinasema mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud ni miongoni mwa wachezajia ambao wanatafutwa na klabu hiyo ya Ujerumani.

Gunners tayari walikuwa wamewasilisha maombi ya kutaka kumchukua Aubameyang mara mbili lakini yakakataliwa na Dortmund.

Aubameyang, 28, alianza kwenye mechi Dortmund kwa mara ya kwanza tangu 16 Desemba mnamo Jumamosi katika mechi ambayo walitoka sare na Freiburg.

Dortmund wamesema wako tayari kumuuza mchezaji huyo lakini iwapo "matakwa fulani yatatimizwa kikamilifu".

Klabu hiyo ya Bundesliga ilikataa ofa ya euro 50m (£43.64m) kutoka kwa Arsenal Jumatano.

Aubameyang alikuwa anatumikia anatumikia adhabu na hakuruhusiwa kucheza mechi yao dhidi ya Wolfsburg wiki mbili zilizopita baada yake kukosa kuhudhuria mkutano wa timu hiyo.

 Mshambuliaji huyo wa Gabon pia aliachwa nje ya kikosi cha klabu hiyo kilichocheza dhidi ya Hertha Berlin wikendi iliyopita kwa sababu maafisa wa klabu walihisi kwamba hakuwa ameangazia mechi hiyo kikamilifu, lakini alicheza dakika 90 katika mechi hiyo dhidi ya Freiburg.

"Tuko tayari kukamilisha uhamisho lakini ikiwa matakwa fulani yatatimizwa kikamilifu," mkurugenzi wa michezo Michael Zorc aliambia runinga ya German TV.

"Tuna msimamo ulio wazi. Arsenal wamefanya majaribio kadha kufikia sasa. Lakini tumeyakataa yote."

Arsenal wanamtafuta Aubameyang kujaza nafasi iliyoachwa na mchezaji wa Chile Alexis Sanchez aliyejiunga na Manchester United mapema mwezi huu kwa kubadilisha na kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan.

Aubameyang, 28, ni stadi sana kwa kufunga mabao na mwandishi wa BBC Stanley Kwenda anasema bila shaka anaweza kufaa klabu hiyo ya England ambayo msimu huu imetatizika kufunga mabao.

Kufikia sasa msimu huu Aubameyang amefunga mabao 13 katika mechi 15 alizocheza.

Alifunga mabao 31 katika mechi 32 msimu uliopita na kwa sasa amepungukiwa na mabao mawili pekee kufikisha mabao 100 aliyoyafunga tangu atue Ujerumani mwaka 2013.

Duru Ujerumani zilikuwa awali zinasema itawagharimu Arsenal zaidi ya £50m kumtoa mchezaji huyo Borussia Dortmund wakifanikiwa.

 Wiki moja iliyopita, mkurugenzi wa michezo wa Dortmund Michael Zorc alisema Wenger aliwakosea heshima kwa kuzungumza hadharani kumhusu mchezaji huyo.

 Wenger alisema nyota huyo wa Gabon anaweza "kuingia sawa" katika klabu ya Arsenal.

Arsenal wakimnunua basi watakuwa wamevunja rekodi yao ya ununuzi wa wachezaji, ambayo inashikiliwa na ununuzi wa Alexandre Lacazette kwa £46.5m.

 Kando na uchezaji, Aubameyang anafahamika sana pia kwa utukutu wake.

Chanzo;- BBC

NATAKA DIAMOND UFANYE KOLABO NA ALIKIBA - MKUBWA FELLA

$
0
0
Said Fella a.k.a Mkubwa Fella ni miongoni mwa jopo la menejimenti ya Msanii mwenye mafanikio barani Afrika Diamond Platnumz amemtaka msanii huyo kufanya collabo na Msanii ambaye ni kipenzi cha watu Alikiba kabla ya meneja huyo hajafa.

Ikumbukwe kuwa kwa zaidi ya miaka 7 sasa kumekuwa na taarifa kuwa wasanii hao wawili ni mahasimu wakubwa na kuwa hawapiki chungu kimoja.

Mkubwa Fella aliitoa kauli hiyo katika tukio la utambulisho wa masanii mpya wa Music Label ya WCB aitwae Mbosso ambaye zamani alikuwa kundi la Yamoto Band.

Bofya hapa chini kumsikiliza Meneja huyo wa Diamond Platnumz alivyoitumia vema kipaza sauti kumuagiza msanii wake kukamilisha collabo hiyo.

SNURA NA ALIKIBA WANATOKA KIMAPENZI?

$
0
0

Hitmaker wa "Moyo Niache"Snura amezifungukia tetesi zilizozagaa kuwa anatoka kimapenzi na mkali wa "Seduce Me"Alikiba.


“Jamani mimi tena mahusiano na Alikiba ha ha ha haaaa…… Hee hizi stori zimetoka wapi jamani mbona kama mmeni-surprise mpaka mimi mwenyewe sasa….kiukweli hii stori mmeni-surprise sana”Snura ameidele The Splash ya Ebony FM akihojiwa na watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji.


Snura ameendelea kukanusha vikali tetesi hizo nakuwataka mashabiki zake kuamini ukweli huu ambao umeuweka wazi.


“Alikiba ni mshikaji wangu tu ambae tumezoeana naye muda mrefu miaka mingi sana, Aaaaah tumezoeana hivyo ni washikaji ni watu ambao labda tumekutana ile tumeongea kawaida kishikaji kirafiki basi hakuna kingine chochote” amesema Snura.

BEKA ATOA SABABU ILIYOMFANYA ASIFIKE KWENYE PARTY YA MBOSO

$
0
0


Msanii wa kizazi kipya bongo Bakari Abdul maarufu kama Beka Flavour ameongea na kuweka wazi sababu kubwa iliyomfanya asihudhurie katika party ya kutambulishwa kwa aliyekuwa mwanamuziki mwenzie waliokuwa wakifanya kazi pamoja katika kundi la ya moto band kabla kundi hilo halijavunjika Maromboso.

Beka anasema sababu kubwa ni kucheleshwa kwa kadi ya mwaliko wa party hiyo, ambapo  siku analetewa kadi ya mwaliko hakuwepo nyumbani alikuwa anashoot video yake mpya, hivyo amerudi ndipo anakutana na kadi na kushindwa kujiandaa kwa muda huo.
"Taarifa niliipata lakini kadi nilicheleshwa kuipata, na ndio ikawa siku anatambulishwa na mimi niko location ya wimbo wangu mpya.nafika nyumbani usiku  nakutana na kadi  yaani ni usiku kwa usiku.kwaio mimi sikuweza kuwahi na kwenda lakini meneja wangu alituwakilisha"amesema Beka.
Hata hivyo Beka anasema kuwa anaamini kabisa kuwa Mboso ni msanii mzuri na ana lengo la kuifisha sanaa ya bongo fleva mbali hivyo nawaomba mashabiki wake wampe sapoti kubwa ili aweze kufanya vizuri.

Mboso na Beka wote walikuwa katika kundi la ya moto kabla halijavunjika , baada ya kuvunjika kila mtu alianza kutafuta ustaarabu wake na kutoka kivyake.hata hivyo wikiendi iliyopita Mboso alikaribishwa rasmi katika lebel kubwa nchini  ya WCB, huku ikitegemewa kuwa wasanii wenzie alikuwa akifanya nao kazi wangeweza kujitokeza kwenye jambo hilo la furaha lakini hali haikuwa kama ilivyo.

Wasanii wengine waliokuwa wakiunda kundi la ya moto kabla ya kuvunjika ni pamoja na aslay na Enock Bella ambao nao pia hawakufika .

MSANII RADIO WA GOODLYFE AFARIKI DUNIA NA HIKI NDIO CHANZO CHA KIFO CHAKE.

$
0
0



Mwanamuziki Moses Ssekibogo ambaye jina la kisanii Mowzey Radio mwenye umri wa miaka 33, kutoka Nchini Uganda amefariki dunia asubuhi yakuamkia leo.


Radio ni miongoni mwa wasanii wanaounda kundi la GoodLyfe akiwa na msanii mwenzake Weasel ambae ni mdogo wake Jose Chameleone.


Umauti umemkuta Radio kufuatia kuvamiwa na kujeruhiwa kichwani akiwa Bar maeneo ya Entebbe wiki mbili zilizopita nakupelekea kufanyiwa oparesheni ya ubongo katika Hospitali ya Casejijini Kampala kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Mulago.


Katika jitihada za kunusuru uhai wake Rais wa Uganda Yowel Museveni alichangia kiasi cha shilingi milioni 30 kwaajili yakusaidia matibabu.



Safari yake ya Muziki ilianza kwa kuwa backing vocal wa Mwanamuziki nguli nchini Uganda Jose Chameleone akishirikiana na msanii wenzake Weasel ambapo baadae mwaka 2008 waliondoka chini ya Usimamizi wa Jose Chameleone, kupitia kampuni yake ya Leone Island Crew nakuanzisha kundi la Goodlyfe.


Baada yakuanzisha kundi lao laGoodLyfe,Radio na Weasel walifanikiwa kupenya katikavituombalimbali vya redio na kitaani kupitia dundo lao la kwanza liitwayo Nakudata walioiachia mwaka 2008.


Tunachukua nafasi hii kuwapa pole ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki na mwenyezi Mungu awape wepesi katika kipindi hiki Kigumu.


Imeandikwa na Chris Bee.

MSANII SPICE DIANA AMLILIA RADIO, NDOTO ZAKE KUTOTIMIA NA AHAIRISHA KUFANYA TAMASHA LAKE.

$
0
0


Mwanamuziki tishio kwa sasa kutoka +256 Uganda Spice Diana alazimika kuahirisha kufanya tamasha lake lililotakiwa kufanyika Februari 2 mwaka huu(leo), kufuatia kifo cha mwanamuziki kutokea kundi la GoodLyfe Radio kilichotokea jana Februari 1 mwaka huu.

Spice Diana ambaye amebahatika kushirikishwa na kundi la GoodLyfe(Radio na Weasel) kupitia dundo liitwalo Kyuma(chuma), ameutumia ukurasa wake wa facebook kueleza namna ukaribu wake ulivyokuwa na Radio sambamba na kutoa taarifa kwa mashabiki zake za kutofanya tamasha hilo.

"Nayakumbuka maneno uliyoniambia kuwa Spice huu ni wako(wangu) na ukaniahidi kuniandikia nyimbo 4 kwa mwaka huu, surprise ambayo ulinitengenezea mbele ya watu waliojitokeza kwenye sherehe yangu ya kuhitimu chuo, na ukanitakia mafanikio mema, Wewe ni mwalimu kwangu, mtu uliyenivutia kuwa mwanamuziki na rafiki yangu mkubwa"amesema Spice Diana.

"Kwa majonzi haya mimi na Uongozi wangu tumelazimika kusitisha kufanya tamasha iliyokuwa ifanyike Februari 2 mwaka huu(Ijumaa), hivyo tutatangaza tarehe mpya yakufanyika kwa tamasha hili hapo baadae baada ya kumpumzisha kaka yetu naamini mashabiki wangu mtaelewa na mwenyezi Mungu atupe wepesi katika kipindi hiki kigumu na ampumzishe kwa amani Kaka Radio" ameongeza Spice Diana.

.

NEW SONG:- ELISHADAI GOLDEN - MAJIBU

$
0
0
Elishadai Golden ni muimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania anakukaribisha kusikiliza wimbo wake mpya uitwao Majibu....... Huu ni wimbo ambao unatoa funzo la kutokata tamaa pindi uwazapo kuwa na jambo jema na hivyo unachotakiwa kumuomba Mola na kungoja majibu.

Karibu sana kuusikiliza.

NEW SONG:- RADIO & WEASEL ft SPICE DIANA - KYUMA

$
0
0
Huu ni wimbo wa mwisho kuachiwa na Marehemu Radio akiwa na msanii wenzake wa GoodLyfe aitwae Weasel wakimshirikisha mwanadada Spice Diana, uliotoka rasmi Januari 26, 2018.

NEW VIDEO:- K.O. - MS2

SIPENDI KUULIZWA KAMA NINA BOY FRIEND:- NINI

$
0
0


Mkali wa dundo la "Niwe Dawa"Nini amefunguka kuwa hapendwi kuulizwa kama ana mahusiano ya kimapenzi na mtu gani kwa sababu ni maisha yake binafsi.

Kauli hiyo ameitoa kupitia The Splash ya Ebony FM wakati akihojiwa na Watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji, baada yakupewa fursa yakuzungumza ni kitu gani ambacho hapendi kuulizwa?.

"Mmmmh kitu ambacho sipendi kuulizwa ni kama nini boyfriend ama sina" amesema Nini ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na mahusiano na Msanii mwenzake Mr Nay a.k.a Ney wa Mitego Boss wa Freenation Records.

Lakini ni sababu zipi zinazomchukiza pindi akiulizwa swali hilo, masanii huyo ambae awali ndoa yake ya mkataba wa kikazi ilivunjika na Recording Label ya MJ records.

"Am sipendi kuulizwa hivyo kwa sababu sijui napenda tu watu wa-concetrate zaidi kwenye kazi kuliko kwenye mambo ya mahusiano, kwa sababu watu wanakuwa wana-concetrate zaidi kwenye mahusiano halafu wanakuwa wanasahau kuwa huyo mtu ana kazi ambazo wanatakiwa wa-concetrate zaidi, kwa hiyo ni suala ambalo sipendi kuulizwa kuwa una boyfriend au unatembea na mtu fulani, sipendi kwa kweli"amesisitiza Nini.

KIONGOZI 'ALIYEIDHINISHA' KIAPO CHA RAILA ODINGA AKAMATWA

$
0
0


 Wakili Miguna Miguna alihusika pakubwa katika kumlisha kiapo cha kuwa 'rais wa wananchi' kiongozi wa Nasa Raila Odinga.

Mwanasiasa aliyejitangaza kuwa kiongozi wa vuguvugu la pingamizi dhidi ya serikali nchini Kenya NRM Miguna Miguna alikamatwa siku ya Ijumaa alfajiri, muda mfupi baada ya kupiga kamsa kufuatia uvamizi wa polisi katika nyumba yake iliopo katika makaazi ya Runda jijini Nairobi.

Mkurugenzi wa kitengo cha ujasusi nchini Kenya George Kinoti alithibitisha kwamba bwana Miguna alikamatwa kwa kutoa kiapo kinyume na sheria mbali na kuwa mwanachama wa vuguvugu la NRM lililopigwa marufuku linalohisishwa na muungano wa Nasa.

''Bwana Miguna alitangaza hadharani kwamba yeye ndio jenerali wa vuguvugu hilo, ambalo tayari limetangazwa kuwa kundi haramu.Wakati alipotangaza hadharani kulikuwa na notisi ya gazeti rasmi la serikali iliotolewa na waziri''.

''Tutamuachaje sisi ni maafisa wa polisi'', alisema Kinoti. ''Pia alisema kwamba atawaongoza watu kuchoma picha za rais Uhuru aliyechaguliwa kidemokrasia. Sasa munatarajia nini kutoka kwetu''?. ''Pia alikiri kwamba ni yeye aliyeongoza kiapo hicho''.

Duru za maafisa wa polisi zimethibitisha kuwa bwana Miguna alipelekwa katika kituo cha polisi cha Kiambu kabla ya kuondolewa na kupelekwa eneo lisilojulikana.

Mapema bwana Miguna alimwambia muhariri wa gazeti la Nation kwamba maafisa wa polisi walivamia nyumba yake mapema alfajiri na kuipekuapekua .

 Wakili huyo ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kumuapisha kiongozi wa Nasa Raila Odinga siku ya Jumanne katika uwanja wa Uhuru Park jijini Nairobi alithibitisha uvamizi huo katika ujumbe uliotumwa saa moja na robo alfajiri Ijumaa.

''Maafisa wa polisi walitumia bomu kuvunja na kuingia katika nyumba yangu. Siwezi kuzungumza katika simu hivi sasa. Wamepekua nyumba yangu'', alisema.

''Wengine wamejificha nje ya nyumba yangu wakitumai nitatoka ili waweze kunipiga risasi na kudai kwamba kulikuwa na ufyatulianaji wa risasi. Sitoki ng'o''.

Majirani walisema kuwa magari kadhaa yalikuwa katika nyumba ya Miguna mapema saa kumi na mbili alfajiri, lakini magari hayo baadaye yakaondoka.

Wafuasi wa Miguna walikuwa wameanza kujaa nje ya nyumba yake na baada ya dakika tano maafisa wa polisi walidaiwa kurusha vitoa machozi ili kuwatawanya.

Wafuasi hao walitoroka na kutazama kwa mbali huku magari ya polisi yaliombeba Miguna yakiondoka.

Baada ya maafisa wa polisi kuondoka , waandishi wa habari waliweza kuingia ndani, na hakukuwa na ishara yoyote ya Miguna huku nyumba hiyo ikiwachwa bila mtu.

RIHANNA KUTOKARIBISHWA NCHINI SENEGAL KWA SABABU HIZI.

$
0
0


Mkali wa dundo la "Love On The Brain"Robyn Rihanna Fenty a.k.a Rihanna anategemewa kuhudhuria mkutano mkubwa nchini Senegal, lakini vikundi vya dini nchini humo wamekataa kumpokea.

"Tumeukataa Ufreemason na mapenzi ya jinsia moja", shirika la vikundi 30 vya kidini wamesema, wakimshutumu muimbaji huyo kwa kutumia ishara za mazo na kuwa mjumbe wa chimbuko la Illuminati, lilanoaminika kuwa ni kundi maalum la watu ambao hudhibiti masuala na uongozi wa dunia na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda Utawala Mpya wa Dunia.

Shutuma hizo zimefutiliwa mbali na wasanii waliowahi kufanya nao kazi huko nyuma, Rihanna atatembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi akiwa katika nyadhifa yake ya balozi wa shirika la elimu 'Global Partnership Foundation'

Shirika hilo lina maadhui wa kuchangisha fedha za kuwafundishia mamilioni ya watoto na vijana katika nchi zinazoendelea.

Chombo cha habari cha Jeune Afrique kimemnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani akisema kuwa atahakikishia usalama washirika wote wa mkutano huo.

NEW VIDEO: MR. NICE – TUHESHIMIANE

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Mr. Nice  ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Tuheshimiane’, video imeongozwa na Pizzo Mtena. Itazame hapa.
Viewing all 911 articles
Browse latest View live