Quantcast
Channel: CHIMBUKO LETU
Viewing all 911 articles
Browse latest View live

MWILI WA RADIO WAWASILI KAGA KWAAJILI YA MAZISHI.

$
0
0





Wadau mbalimbali wa muziki nchini humo pamoja na Afrika mashariki wanatarajia kuhudhuria mazishi hayo.

Mwili wa mwanamuziki wa Kundi la Goodlyfe, Mowzey Radio umewasili kijijini kwa mama yake,
Kaga asubuhi hii kwaajili ya shughuli za mazishi mchana wa leo.


Muimbaji huyo wa Uganda alifariki Alhamisi hii akiwa katika hospitali ya Case ya nchini humo baada kudaiwa kushambuliwa na baunsa na kusababishiwa kuvunjika fuvu la kichwa pamoja na uti wa mgongo
.
Picha kwa hisani ya News Vision Uganda

NEWS SONG:- MR. P - MY WAY

NEW VIDEO:- BRIGHT - SINA

NEW VIDEO:- CINDY SANYU ft SKALES - ONE BY ONE

NEW VIDEO:- GENEVIEVE - HOI

MSANII YCEE AVUNJA MKATABA NA SONY, JE ALIKIBA KUFUATA?

$
0
0


Racord Label ya Tinny Entertainment inayomsimamia mkali wa kibao cha Omo Alhaji Ycee wa Nchini Nigeria, imefikia uamuzi wa kuvunja mkataba wake na kampuni ya Sony Music tawi la Afrika Magharibi kwa madai kuwa mkataba huo unawanufaisha Sony zaidi.

Kupitia maelezo ya barua ya Tinny Entertainment, inafafanua kwamba Sony wameshindwa kutimiza malengo yao ya kuuvusha muziki wa Ycee kimataifa(global), licha ya Sony kupewa jukumu la kusambaza kazi zake kupitia music platforms mbalimbali ulimwenguni.

Sakata hili linajiri ikiwa ni kipindi cha mwaka mmoja hadi sasa tangu Tinny Entertainment wasign dili nono na Sony la kuwa wasambazaji wakuu wa kazi za Ycee.

SERIKALI KUBORESHA MAFUNZO KWA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
 
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuboresha Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi vya Watu wenye Ulemavu ili kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri na kupata ujuzi mbadala wa kumudu maisha yao.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu) Stella Ikupa leo Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi Mhe. Oscar Mukasa lililohusu umuhimu wa kuwatazama vijana wenye ulemavu mbalimbali kwa namna ya kipekee.

Mhe. Ikupa amesema kuwa Serikali inatambua Vijana wenye ulemavu kuwa ni kundi mojawapo miongoni mwa watanzania wenye ulemavu ambalo linakabiliwa na changamoto mbalimbali.

“Kwa kutambua umuhimu wa kundi hili la watu wenye ulemavu wakiwemo vijana, Serikali iliunda Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu ambalo kazi yake kubwa ni kutoa ushauri kwa Serikali na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya watu wenye ulemavu juu ya namna bora ya kushughulika na changamoto zao zikihusisha zile za kundi la vijana wenye ulemavu,” amefafanua Naibu Waziri Ikupa.

Aidha, Mhe. ikupa amesema kuwa Serikali imeendelea kuunda kamati za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri ya Wilaya, Kata na Mtaa kwa lengo la kuhakikisha masuala ya watu wenye ulemavu yanazingatiwa ili kuondokana na kero mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu Elimu, Afya, Ajira na Mikopo ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Hata hivyo, Naibu Waziri Stella Ikupa amewahimiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia ipasavyo utekelezaji wa suala hilo ambalo liko kisheria na pia ametoa wito kwa Wakurugenzi hao kuhamasisha walemavu kujiunga kwenye vikundi mbalimbali ikiwemo vikundi vya vijana.

TIBA MTANDAO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisisitiza jambo kwa wataalamu wa sekta ya afya wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga, akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa tiba mtandao nchini kwa wataalamu wa sekta ya afya (hawapo pichani) wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Peter Phillip Mwasalyanda (aliyeketi katikati), akisikiliza kwa makini kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma
Wataalamu wa sekta ya afya wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya (hayupo pichani) wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma

Serikali imejipanga kutumia tiba mtandao kuboresha huduma za afya nchini kwenye hospitali zote za ngazi ya taifa, rufaa na wilaya ili kuwawezesha wagonjwa waishio sehemu mbali mbali nchini kupata huduma za afya kwa wakati na kwa ufanisi.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akifungua kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la LAPF, Dodoma.

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha watendaji wakuu wa hospitali za taifa nchini, madaktari bingwa wa sekta ya Afya, wakuu wa taasisi zinazoshughulika na sekta ya Afya, Wizara ya TAMISEMI, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; taasisi nyingine za Serikali; sekta binafsi na wabia wa maendeleo ili kujadiliana na kuwa na uelewa wa pamoja wa kufanikisha utekelezaji wa huduma za tiba mtandao ili kuboresha huduma za afya nchini.

Amesema kuwa tiba mtandao itawezesha na kuongeza ufanisi katika kufanya uchunguzi, utoaji wa tiba na madawa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na yanayotokana na ajali za barabarani. “Hadi hivi sasa ni asilimia 37 tu ya wagonjwa wa kifua kikuu ndio wanaotambulika na kupatiwa huduma na Wizara ya Afya katika hospitali mbalimbali nchini. Hivyo, tiba mtandao itawezesha upatikanaji wa wagonjwa na ufikishaji wa huduma kwao kwa wagonjwa wengine asilimia 63”, amefafanua Dkt. Ulisubisya.

Ameongeza kuwa tiba mtandao itapunguza gharama za wagonjwa na wanaowahudumia kusafiri kufuata madaktari. Aidha, amewataka wakuu hao wa taasisi kuwaruhusu wataalamu wao, wa Wizara ya TAMISEMI na wa Wizara ya Afya, kushiriki mafunzo ya tiba mtandao ili kuongeza ufanisi wao katika kuhudumia wagonjwa.

Amewataka wataalamu wa afya na wakuu wa taasisi zinazohusika na masuala ya afya kununua vifaa tiba vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) vyenye viwango na ubora unaohitajika ili kuwezesha tiba mtandao na manunuzi hayo yazingatie na kufuata ununuzi wa pamoja wa huduma na bidhaa za Serikali. 

Vifaa vya kisasa vya TEHAMA vinavyohusika na tiba mtandao vitawawezesha wataalamu kufanya uchunguzi kwa mgonjwa, kupata majibu ya uhakika na kumpatia mgonjwa tiba inayostahili na ya uhakika. Aidha, amemuelekeza Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Ulanga, ambao ndio waanadaji na waratibu wa kongamano hilo, kushirikiana na TTCL kuhakikisha kuwa tiba mtandao inapatikana katika hospitali zote za rufaa na hospitali ambazo zina changamoto ya kijiografia ya kufikika kwa urahisi. Aidha, hadi hivi sasa huduma ya tiba mtandao inapatikana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bagamoyo, KCMC-Moshi, Bugando-Mwanza na Benjamin Mkapa, Dodoma. 

Naye Eng. Ulanga amesema kuwa UCSAF imeanzisha huduma ya tiba mtandao kwenye vituo 14 vya majaribio. Aidha, imeainisha orodha ya vituo 279 ikiwa ni pamoja na hospitali za taifa, rufaa na wilaya ambazo zitaunganishwa na kuwezeshwa kutoa huduma ya tiba mtandao nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam Dkt. Julius Mwaiselage, akiwa mmoja wa washiriki wa kongamano hilo amesema kuwa, tayari tulikuwa tunatumia huduma ya tiba mtandao kwa wagonjwa wetu kwa kushirikiana na hospitali nyingine zilizopo nchini India kwa kuwafanyia wagonjwa uchunguzi na kuona kama kweli mgonjwa husika anahitaji kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi. 

“Uwepo wa huduma ya tiba mtandao kwenye hospitali zetu nchini, itatuwezesha kufanya uchunguzi na kutoa tiba kwa wagonjwa waliopo mikoani hivyo kuwapunguzia gharama wagonjwa za kuja Dar es Salaam na endapo watalazimika kuja basi watakaa kwa muda mfupi ukilinganisha na hapo awali”, amesema Dkt. Mwaiselage. Washiriki wengine wa kongamano hilo ni kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bugando, MOI, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kiwete, Mloganzila, Aga Khan, Hospitali ya Rufaa Mbeya, NHIF, PATH na Shirika la Afya Duniani.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAELFU YA WATU MAZIKO YA MWANASIASA MKONGWE MAREHEMU MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mara baada ya kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa akiweka shada la maua katika kaburi  la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye Kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Wajukuu wa marehemu pamoja na wafiwa wengine wakiwa katika hali ya majonzi makaburini hapo. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waombolezaji mara baada ya maziko ya marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

HAYA NDIYO MAMBO YANAYOWEZA KUKUVUNJIA HESHIMA

$
0
0
HAKUNA kitu kibaya maishani kama kuonekana upo katika daraja la chini na mtu wa kudharaulika kwenye jamii unayoishi. Kisaikolojia kuna madhara makubwa.
Ni imani yangu kuwa kila mwanadamu timamu anapenda kuheshimiwa lakini wengi wetu tunashindwa kupata heshima tunayoitaka kwa sababu hatufahamu jinsi ya kuishi mbele ya wenzetu.

Kitaalamu, hakuna jambo ambalo hutokea maishani bila sababu maalumu hivyo hata kudharauliwa kwako au kwetu ndani ya jamii tunayoishi kunatokana na jinsi tunavyoenenda.
Mwalimu wangu wa somo la maisha na saikolojia, Eric Shigongo, aliwahi kuniambia ‘Nothing happens in the sky, but the elements should be there,’  akimaanisha kuwa hakuna kitokeacho angani pasipo kuwa na dalili au sababu zake.
Naomba nianze kutoa njia za kukusaidia kurejesha heshima yako kwa kuperuzi na wewe baadhi ya dokezo muhimu zinazoweza kukusaidia kujitambua na kuweza kuyaepuka maisha ya kudharauliwa.

MUONEKANO
Kwanza kabisa ni jinsi unavyoonekana. Muonekano ninaouzungumzia hapa ni usafi wa mavazi na mwili kwa ujumla. Hata siku moja hakuna mchafu anayeheshimika katika jamii anayoishi hata kama ana kipaji kikubwa kiasi gani.
Kwa hiyo uchafu wa mavazi na mwili huchangia mtu kudharauliwa katika jamii anayoishi. Linaweza kuwa jambo dogo sana lakini ni moja kati ya sababu kubwa inayochangia kuporomoka kwa thamani yako mbele ya wenzako.

Mazungumzo
Hapa naomba nieleweke kuwa unachokizungumza kinaweza kukujengea heshima au kukubomolea heshima. Kauli zisizo na busara zitakufanya udharaulike kwa kila mtu. Uropokaji usiokuwa na mantiki huchangia kuporomosha heshima yako hasa kama utakuwa muongeaji zaidi. Biblia inasema penye wingi wa maneno hapakosi uovu.

UTENDAKAZI WAKO
Ndugu zangu, siku zote heshima ya mtu ni kazi. Watu wengi hawapendi kufanya kazi kwa bidii huku wengine wakijiendekeza kwa tabia ya kuombaomba, jambo hilo halifai kwa vile huchangia kubomoa heshima yako mbele ya jamii. Fanya kazi usiishi bila kujishughulisha.

KUTOTIMIZA AHADI
Kama una tabia za kuahidi mambo halafu unashindwa kuyatekeleza, basi unajiweka katika nafasi mbaya ya kutunza heshima yako katika jamii unayoishi. Bora ukwepe kutoa ahadi kuliko kuahidi na kutotimiza.

SIFAZISIZO NA MAANA
Nakumbuka msemo mmoja kutoka kwa mwandishi mwandamizi aliyekuwa mtaalamu wa falsafa za maisha, marehemu Adolf Balingilaki, ambao unasema kwamba:
“Ukitafuta heshima kwa gharama ya juu, basi utalipwa dharau kwa bei nafuu.”
Msemo huu unamaanisha nini? Siku zote ukiwa unafanya mambo yako kwa ajili ya kusifiwa au mazungumzo yako kuwa ya kujiinua, watu watakudharau.

KUTOKUWA MWAMINIFU
Suala la uaminifu ni pana, kuna uaminifu wa fedha, siri, dhamana na mambo kama hayo, hivyo ni vema kila unachoaminiwa lazima ukitunze kwani ukiwa mtu wa kuvunja uaminifu fahamu kuwa utashusha heshima yako.

MATANGAZO YA VITUO VIWILI VYA TELEVISHENI NCHINI KENYA YAREJEA HEWANI.

$
0
0
NTV, Citizen na KTN zilifungwa kwa madai kuwa vilipanga kupeperusha matangazo ya moja kwa moja ya kuapishwa kwa Raila Odinga.

 Matangazo ya vituo viwili vya televesheni Kenya, KTN na NTV yamerejea hewani baada ya kufungiwa siku 7 na serikali. 

Lakini bado haviwezi kutazamwa na Wakenya wengi ambao hawana king'amuzi. 

Kupitia mtandao wao wa Twitter, NTV wamesema wamerudi hewani kwenye ving'amuzi vya "Dstv, GoTV and Zuku baada ya kufungiwa na serikali."

Stesheni ya iliyokuwa mmojawapo zilizoathirika na hatua ya serikali ,Citizen TV bado haijafunguliwa. 

Serikali ilizifunga stesheni tatu za televisheni NTV, Citizen na KTN kwa madai kuwa vilipanga kupeperusha moja kwa moja matangazo sherehe ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama rais licha ya onyo kutofanya hivyo.

 Awali, wanaharakati waliokuwa wakiandamana kuishinikiza serikali kuvifungua vituo hivyo, walitawanywa na polisi kwa kutumia gesi ya kutoa machozi.

"Hii si mara ya kwanza tumiona serikali ya Jubilee ikiangamiza haki za waandishi wa wahabari. Tumeona ikifanyika kwa muda mrefu".

Tom Oketch mmojawapo wa waandalizi wa maaandamano hayo ameiambia BBC .

"Hawa heshimu sheria, hawa heshumi katiba, wananchi wa Kenya hawatawaruhusu kuturidisha katika enzi za Jomo Kenyatta, enzi za Moi, tutapigana nao mpaka mwisho" ameelezea Tom.

Wiki iliyopita,Mahakama Kuu nchini humo iliamuru kuwashwa kwa vituo vya habari hivyo vitatu na serikali na kuiagiza serikali kutoingilia utendaji kazi wa vituo hivyo hadi kesi hiyo itakaposikilizwa kikamilifu.

MIMI NI MVIVU SANA WA KUTAFUTA IDEA LAKINI NAANDIKA SANA:- MR BLUE

$
0
0


Licha ya mwanamuziki Mr Blue kufanya vizuri kwenye Bongoflava kwa muda wote toka alivyoingia kwenye muziki lakini ataja mapungufu yake.

Hitmaker huyo wa "Mbwa Koko" ameweza kushare mapungufu yake hayo kwa mashabiki wake wakati akizungumza katika The Splash ya redio Ebony FM akihojiwa na watangazaji Chris Bee na Fredoo.

"Kiukweli siri ya mafanikio ya uandishi wangu toka nianze game nikuangalia sana suala la ubunifu.....aaaaah naangalia sana ubunifu naangalia nini wanataka watu naangalia sana ideas"amesema Mr Blue.

"Mimi kwenye kuandika nyimbo kidogo sio mgumu sana lakini kwenye kutafuta idea ni mgumu sana huwa naangalia sana idea yakuandikia nyimbo"ameongeza Mr Blue.

GOSPEL VIDEO:- HASHIM CHAZ - NIPO KITANDANI

SAMATTA AKARIBIA KUTWAA TAJI ULAYA, GENK YATINGA FAINALI KOMBE LA UBELGIJI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, GENK
NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza kwa dakika zote 90 na kuisaidia klabu yake, KRC Genk kutinga fainali ya Kombe la Ubelgiji kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Kortrijk katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
 Kwa matokeo hayo, Genk inasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya sare ya 3-3 kufuatia awali kufungwa 3-2 kwenye mchezo kwanza Uwanja wa Guldensporen mjini Kortrijk.
 
Mfungaji wa bao pekee la Genk usiku wa jana ni kiungo Msenegali mwenye umri wa miaka 28, Ibrahima Seck aliyefunga dakika ya 15 akimalizia pasi ya kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero.
Mbwana Samatta akienda hewani kupiga mpira dhidi ya wachezaji wa Kortrijk katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali Kombe la Ubelgiji jana  
Mbwana Samatta akipambana na beki wa Kortrijk katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena jana

Genk sasa itakutana na mshindi wa jumla kati ya Club Brugge na Standard Liege zinazomenyana kesho Saa 4:45 usiku Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge. Mechi ya kwanza Standard Liege ilishinda 4 – 1 na leo itakwenda kupigania sare au kufungwa si zaidi ya 2-0.
 Samatta jana alikuwa anacheza kwa mara ya nne tangu apone maumivu ya mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia iliyochanika Novemba 4, mwaka jana akiichezea KRC Genk ikilazimishwa sare ya 0-0 na Lokeren katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk na kumsababisha afanyiwe upasuaji mdogo. 
 Kwa ujumla Samatta amefikisha mechi 74 tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
 Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Uronen, Colley, Aidoo, Nastic, Wouters, Seck, Pozuelo/Writers dk79, Samatta, Buffel na Ingvartsen/Karelis dk65.
 KV Kortrijk; Kaminski, Kumordzi, Makarenko, Kagelmacher, Rougeaux, Ajagun/Lepoint dk73, Chevalier, Van Der Bruggen/Azouni dk73, Ouali/Stojanovic dk84, D'Haene na Perbet.

SHETTA WA SASA NI MWENYE KUSUJUDI VITU VYENYE UBORA NA VIKUBWA:- MX CARTER

$
0
0


Meneja wa wasanii na Wakala wa YouTube Tanzania kupitia kampuni ya Ngoma, Mx Carter amemzungumzia Shetta kuwa ni mwanamuziki aliyepevuka kifikra na kimuziki.

Kauli ya Mx Carter imekuja baada yakuanza kufanya kazi na Shetta na kwamba kwa sasa msanii huyo anataka vitu vyenye ubora katika muziki.

"Tofauti ya Shetta sasa hivi.....Shetta kwanza hataki kurudi nyuma, Shetta akimuambia afanye kitu kwa kubahatisha anakuwa hawezi kufanya tena" amesema Mx Carter

"So Shetta wa sasa hivi anataka quality,Shetta wa sasa hivi anataka audio nzuri,Shetta wa sasa hivi anataka vitu vikubwa yaani na tumejipanga kwa hilo kwa hiyo watu watarajie vitu vikubwa kwa Shetta" ameongeza Mx Carter.

TAZAMA VIDEO YA SHETTA ft G NAKO - VUMBA

KUMBE DIAMOND PLATNUMZ ANASHUSHWA KIMUZIKI NA MTU/WATU MENEJA WAKE AANDIKA.....

$
0
0


Lisemwalo lipo kama halipo basi linakuja, Nani anayetaka kumshusha Diamond Platnumz? Ukiachana na Speculations zote lakini lazima tu kutakuwa na jambo kubwa behind this saga.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Meneja wa Diamond Platnumz...... Sallam Sk ameandika ujumbe wenye shutuma nzito na wenye kumlenga mtu/watu.
  • sallam_skKumbe tatizo ni kumpoteza huyu kijana?????? Waambie familia yako na wazazi waliyokuleta katika haya maisha huyu MTOTO kaletwa kwa makusudi maisha haya, ili kuleta ukombozi ya dhulma uliyokuwa unaleta kwenye Taifa hili, unatikiwa kujua Kwanza hili Taifa sasa Rais anaitwa John Pombe Magufuli.

SISI HATUNA BIFU NA SUATI SOUL TUNAHESHIMU MUZIKI NA HARAKATI ZAO:- GABU P-UNIT

$
0
0


Mwanamuziki kutokea +254 Kenya Gabu ambae ni crew member wa kundi la P - Unit kafunguka kuwa hawana ugomvi Kundi tishio kwa sasa barani Afrika Sauti Soul  lenye masikani yake nchini humo.

Kwa muda mrefu kumekuwepo na porojo kuwa P Unit wanawahofia Sauti Soul hali inayopelekea kushindwa kurudi mpaka sasa baada ya kusitisha kufanya kazi kwa pamoja kwa P Unit baada ya ukimya uliosababisha Kundi la Sauti Soul ku-take over.

Msikilize Mkali huyo wa He we Go, Gabu wakati akihojiwa na Kituo cha redio AFM cha Mkoani Dodoma.

NEW VIDEO:-PATORANKING - AVAILABLE

NEW VIDEO:- CASHMERE CAT, MAJOR LAZER, TORY LANEZ - MISS YOU

COUTINHO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO BARCA YATINGA FAINALI KOMBE LA MFALME

$
0
0

Kiungo Mbrazil, Philippe Coutinho akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 49 Uwanja wa Mestalla mjini Valencia.

Coutinho aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Andre Gomes katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme. 

Hilo ni bao la kwanza kwa Coutinho tangu asajiliwe mwezi uliopita kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 145 kutoka Liverpool wakati bao la pili lilifungwa na Ivan Rakitic dakika ya 82 na wote walifunga kwa pasi za Luis Suarez. 

"Najisikia furaha sana kufunga Goli langu la kwanza Barcelona na kuweza kuisaidia timu kwenda Fainali"amesema Coutinho.
Barca inaingia fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya Februari 1 kushinda 1-0 Camp Nou bao la Suarez pasi ya Lionel Messi dakika ya 67 na sasa itakutana na Sevilla iliyotoa Leganes kwa jumla ya mabao 3-1, sare ya 1-1 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.

Tazama picha zaidi hapa Chini.
 Coutinho akifurahia goli lake la kwanza Barca
 Messi akifurahi na kumpongeza Coutinho.
 Coutinho akimshukuru Mola baada ya kuifungia Barca goli la kwanza.
 Wachezaji wa Barca wakifurahia kwa pamoja goli la kwanza na Coutinho klabuni hapo.
Viewing all 911 articles
Browse latest View live