Quantcast
Channel: CHIMBUKO LETU
Viewing all 911 articles
Browse latest View live

ALBAMU YA VANESSA "MONEY MONDAYS" NA VIPANDE ADIMU

$
0
0
Pumzi ya Mwisho ikiwa ni track Namba 8 kwenye Album ya Vanessa Mdee moja ya track iliyomuweka Vee money katikati ya Marappers wawili wakali mmoja kutoka Bongo Joh Makini na mwingine toka Bondeni(Afrika Kusini)  Cassper Nyovest.

  Ndio maana hutoshangaa kuona Vee naye kuchana humo ndani ila ukifuatilia ni sababu ya ufundi wa vichwa viwili vilivyosimama naye, Cassper akidhihirisha kweli yeye ndo rapa bora Afrika, Joh naye akiwa kapambana asifunikwe.

Nyimbo inaleta mvuto wakipekee, yote hiyo utaipata kwenye #MoneyMondays
#albumreview
#collabos
 
Written by @deotrump_

PATA BURUDANI YENYE NYIMBO 6 KUTOKA KWA MASANII CHRIS BEE NA HAUTOJUTA.

$
0
0
Sasa waweza kujipatia..... Nyimbo za Mwanamuziki Chris Bee...... Kupitia BOOMPLAY MUSIC APP........ Kwa kubofya LINK hii www.boomplaymusic.com/share/artist/886895
 

Baada ya hapo Download App ya BoomPlayMusic......ili upate nafasi ya kuzisikiliza kwa urahisi. na kama tayari umekwisha kuipakua App hiyo itakupeleka moja kwa moja kusikiliza nyimbo hizo.......
.
.
HII NDIO ORODHA KAMILI YA NYIMBO HIZO.
1. Chris Bee ft Dullayo - Diva.... Produced by Zuzu
2. Chris Bee - Safari......Produced by Zuzu
3. Chris Bee ft Petronia - Bashee.......Produced by Father Beat.
4. Chris Bee ft Neylee - Urudi.......Produced by Fraga
5. Chris Bee ft G Sacha & Sylvia - Walawala........Produced by Fraga
6. Chris Bee ft Sam Flavour, Fraga & Sylvia - Walawala remix........Produced by Fraga

DORTMUND: HAKUNA MAZUNGUMZO YA KUMUUZA AUBAMEYANG

$
0
0


Mkufunzi wa Borussia Dortmund Peter Stoger anasema kuwa hakuna ombi la kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang lililowasilishwa na Arsenal.

Mshambuliaji huyo wa Gabon ambaye ananyatiwa na the Gunners, hakusafiri na wachezaji wenzake kwa mechi ya Ijumaa dhidi ya Hertha berlin ambayo ilikamilika 1-1.

"Hakuna mazungumzo yoyote katika meza kuhusu uhamisho wa Aubameyang ,yanayoendelea ni uvumi" alisema Stoger.

"Tunapanga na Pierre-Emerick Aubameyang na kuna vile atakavyorudi katia kikosi cha kwanza cha timu ."  Stoger ameongeza.

 Aubameyang pia alikosa mechi ya Jumapili iliotoka sare ya 0-0 dhidi ya Wolfsburg baada ya kukosa kuhudhuria mkutano wa timu.

 Mchezaji huyo mwenye urmi wa miaka 28 ni mshambuliai wa Dortmund mwenye magoli mengi msimu huu akiwa na mabao13 katika mechi 15 .

Chanzo:- BBC

JOSE MOURINHO: NINASUBIRI HABARI NJEMA ZA KUMSAJILI ALEXIS SANCHEZ

$
0
0


Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amethibitisha kwamba klabu hiyo iko katika meza ya mazungumzo ya kumsajili shambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez na kwamba anasubiri habari njema.

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji huyo wa Chile akajiunga na wapinzani wao katika ligi ya EPL.

Kiungo wa kati wa United Henrikh Mkhitaryan anatarajiwa kujumlishwa katika makubaliano hayo na kwamba hakuorodheshwa katika kikosi kitakachokabiliana na Burnley.

Hakuna haja ya kuficha ama kukataa lakini hatujaafikiana makubaliano.

 Najua kwamba kila mtu anajua tuko katika meza ya mazungumzo na hususana baada ya mkufunzi wa Arsenal kuzungumza wazi.sanchez mwenye umri wa miaka 29 hayoko katika kandarasi na Arsenal mwezi Juni na andaiwa kuingia mkataba wa kibinafsi na klabu hiyo ya Old Trafford.

MBALI NA GHETTO KIDS, RAPPER OCTOPIZZO NAE APEWA MWALIKO WA KUHUDHURIA TUZO GRAMMY MAREKANI

$
0
0


Wakati wadau na mashabiki wa muziki Afrika Mashariki wakisubiria kwa hamu performance kali ya Kundi bora la dance Ghetto Kids kutoka Uganda, kwenye jukwaa la Grammy Awards 2018 wakiwa sambamba na Rapper French Montana kupitia ngoma ya Unforgettable.

Habari njema ni kwamba Rapper kutoka Kenya Octopizzo amepata mualiko "Invitation" kuhudhuria kwenye event kubwa ya utoaji tuzo za Grammy Awards New York, USA.

Octopizo atawakilisha East Africa kwenye event hiyo itakayofanyika January 28. Na kupitia ukurasa wake kwenye Mtandao wa kijamii wa Instagram ameweza kushare taarifa njema kwa mashabiki wake.

NEW VIDEO| YOUNG TUSO FT MR BLUE | KAZA ROHO | WATCH

$
0
0
Hii ni video ya kwanza kabisa katika Career ya Msanii Young Tuso, toka kuingia kwake kwenye Gemu la Muziki wa kizazi kipya. Itazame hapa.

NEW VIDEO| MR. BLUE | MBWA KOKO | WATCH

$
0
0
Mwanamuziki mwenye uwezo Mkubwa wa Ku Rap na kuimba Mr Blue, aunza mwaka 2018 na Mbwa Koko.......... Enjoy.....


NEW VIDEO: NAMELESS – VOLOYOOM (VOLUME)

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Nameless ameachia video ya ngoma yake mpya iitwayo ‘Voloyoom’ (volume) Audio ya ngoma hiyo imeteyarishwa na Mainswitch studios na upande wa video imeongozwa na VJ ONE.

NIMERAHISISHIWA KAZI SASA HIVI KAZI YANGU KUBWA NI KUREKODI TU:- LADY JAYDEE

$
0
0


Malkia wa Muziki wa Kizazi kipya Tanzania(BongoFlava) Lady Jaydee, aeleza namna atakavyonufaika na mkataba mpya aliosaini na Record Label ya Taurus Musik ya nchini Kenya. 

Ikumbukwe kuwa Mnamo Novemba 27, mwaka 2017 Taurus Musik iliingia makubaliano maalumu yakuwasimamia wasanii wawili akiwemo Lady Jaydee na Msanii mwenye asili ya Congo DRC Alicious.

"Mkataba mpya niliosaini niwa albums tatu, kila mwaka natakiwa kutoa albamu mmoja kwa hivyo na namna tunavyofanya kazi na hii Record label ni kitu tofauti na watu wengine ambao nimewahi kufanya kazi nao" amesema Lady Jaydee.

Mkali huyo wa Ngoma ya Baby Lady Jaydee, huku akiwa mwenyefuraha hajasita kuwajuza mashabiki wake namna atakavyonufaika zaidi na mkataba huo.

"Wana-invest pesa yao, wanaweka pesa kwenye kila kitu wanakulipia studio, wanakulipia audio tofauti na watu wengine ambapo unaweza kuwa unafanya nao kazi lakini inabidi wewe ndio u-invest utoe hela yako mfukoni" ameeleza Lady Jaydee.

"Na ninaona kwamba kitu ambacho kitaweza kutokea na hii record label mpya ni kwamba mtu hawezi akaweka pesa yake akakubali ipotee kwa hiyo watafanya kila njia kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kwamba pesa yao inarudi wanapata faida na mimi napata faida" ameongeza Lady Jaydee.

Hata hivyo amemalizia kwa kueleza unafuu utakaokuwepo na kujivunia kuwepo chini ya Usimamizi wa Taurus Musik Record Label.

"Tofauti na ambavyo ilikuwa mimi naweka pesa yangu, kwa hiyo inabidi mimi ndio ni hustle hata kama mtu mwingine nafanya nae kazi lakini hawezi kusikia uchungu kwa sababu sio pesa yake hii ndio tufauti ya Record label mpya hii nayofanya nao kazi sasa hivi na watu wengine ambao nimewahi kufanya nao kazi hapo nyuma" amehitimisha Lady Jaydee.

GEORGE WEAH KUAPISHWA LEO KUWA RAIS WA LIBERIA

$
0
0
Raia wa Liberia wanasubiria kwa hamu tukio hilo la kuapishwa kwa Rais wao George Opong Weah,ambapo wamekesha katika uwanja wa mpira wa taifa,mahala ambapo leo historia ya mwanasoka huyo inajiandika upya kutoka kung'ara katika soka na hatimaye kuingia katika uga wa siasa kuwa rais wa taifa hilo lenye historia ya milima na mabonde kisiasa.

George Weah, maisha yake ya utoto,yalikuwa katika mazingira duni katika mji mkuuwa Liberia Liberia Monrovia, alipata mafanikio makubwa katika medali ya soka na kufanikiwa kuchezea timu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Chelsea na AC milan. 
 
Ni Muafrika pekee kuwahi kushinda tuzo mchezaji bora wa FIFA na tuzo ya Ballon.

Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa maseneter katika bunge la Liberia. 

Aligombea urais mwaka 2005 ,na Alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini kashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki katika duru ya pili.

Aliyewahi kuwa meneja wa George Weah katika klabu ya Monaco inayocheza ligi kuu ya Ufaransa Arsernal Wenga amealikwa na atakuwepo katika uapisho huo.

Meneja huyo wa Arsenal alikuwa meneja wa Weah katika klabu ya Monaco inayocheza Ligi Kuu ya Ufaransa miaka ya 1990 na amesema hakuwahi kufikiria kwamba wakati mmoja mchezaji huyo angekuwa rais.

Huyu ndiye George Opong Weah ambaye leo anaapishwa kuiongoza Liberia.

Chanzo:- BBC

MIUNGU WA WAHINDI WANA RANGI GANI?

$
0
0
 Mmoja ya miungu ya Kihindu Sita akiwa pichani na watoto wake mapacha Luv na Kush 

Nchini India ambapo ngozi nyeupe inasifiwa, vuguvugu jipya limeibuka na kuitazamia miungu wa Wahindi kuwa na rangi nyeusi zaidi.

Upendeleo wa ngozi nyuepe si kitu kipya nchini India na kwa miongo mingi, kuwa na ngozi nyeupe kunatafsiriwa bora zaidi.

Mafuta yanayochubua ngozi ni miongoni ya vipodozi vinavyouza zaidi nchini humo na waigizaji vinara wakike na wakiume wa Bollywood wanaonekana mara kwa mara kwenye matangazo ya vipodozi vinavyogeuza ngozi kuwa nyuepe zaidi.
 Mwanamitindo Suruthi Periyasamy alifurahi sana alipoitwa kumuigiza mungu wa utajiri Lakshmi

Miaka ya hivi karibuni, aina tofauti ya mafuta yamezinduliwa yanayodai kufanya nywele za kwapani kuwa nyeupe pamoja na sehemu za siri za wanawake, na matangazo yanawashawishi wateja kuamini kuwa muonekano wa ngozi nyeupe itasaidia kuboresha maisha yao kwa kupata kazi nzuri zaidi au kushinda mapenzi ya mtu wanaompenda.

Hivi karibuni,kumekuwa na kampeini kama "Dark is Beautiful" au Uweusi ni Urembo na "unfairandlovely" zinazotoa wito kwa watu kusherekea ngozi nyeusi. 

Hata hivyo upendeleo huo wa ngozi nyeupe bado umeendelea, na muongozaji wa filamu za matangazo, Bharadwaj Sundar anasema upendeleo huo hauishii kwenye viumbe vya ulimwengu bali upo pia kwenye viumbe vya mbinguni.
 Krishna, mmoja ya miungu anayetafsiriwa katika vitabu vya dini ya Kihindu kuwa na ngozi nyeusi naye pia anaonesha mara kwa mara akiwa na ngozi nyeupe 

"Picha zote za miungu maarufu tunazozioana, picha katika kuta zetu nyumbani na sehemu za ibada, kwenye mabango madukani na makalenda yote yanawaonesha wakiwa na ngozi nyeupe."

Bw Sundar anaelezea hata Krishna, mmoja ya miungu anayetafsiriwa katika vitabu vya dini ya Kihindu kuwa na ngozi nyeusi naye pia anaonesha mara kwa mara akiwa na ngozi nyeupe.

"Kila mtu hapa anapendelea uweupe. Lakini mimi nina ngozi nyeusi na rafiki zangu wote wanangozi nyeusi pia. Kwa hio nitahisije ukaribu na miungu wenye ngozi nyeupe?" 

Kujaza pengo hili, Bw Sundar anayeishi kwenye mji wa Chennai kusini mwa India, pamoja na mpigapicha walibuni "Dark is Divine" au Uweusi ni Ubora - mradi unaoonesha miungu ya kihindu kuwa na ngozi nyeusi.
 Durga is almost always portrayed as a fair-skinned goddess 

Waliwaleta wanamitindo wenye rangi ya ngozi nyeusi na kuwavalisha kama miungu na kuwapiga picha ndani ya siku mbili mwezi Disemba, matokeo yao ni ya kustaajibisha.

Tangu kampeini hio kuzinduliwa mwezi uliopita,Bw Sundar anasema amepokea simu nyingi and watu wamepokea kazi yake vizuri sana japo kuna baadhi ambao wamewashutumu kuwa na uonevu wakisema kuwa mungu Kali kwa muda mrefu amekuwa akioneshwa akiwa na ngozi nyeusi.
Mtoto Krishna ni miongoni wa miungu maarufu katika dini ya Kihindu 
 
Bw Sundar anasema yeye ni Mhindu aliyeshika dini na hakukusudia kutoheshimu mtu, lakini "tukiangalia kote, tunapata kwamba mara asilimia 99.99, miungu wetu wanangozi nyeupe"

"Muonekano inasehemu kubwa katika namna ambavyo tunachukulia watu, hasa wanawake, tiliona ni jambao ambalo lazima tulizungumzie" ameelezea.

" Na kupitia mradi huu, tunajaribu kuikosoa imani ya kwamba uweupe ni ubora"

TYGA ATANGAZA UJIO WA ALBAMU YAKE MPYA

$
0
0


Tyga allianza mwaka 2018 kwa kuachia ngoma iitwayo ‘Temperature’ na kisha akatushushia remix ya ‘Ric Flair Drip’ akimshirikisha Offset.

Leo msani huyo anayeishi huko jjini Los Angels nchini Marekani ametangaza kuachia albamu mpya inayoitwa KYOTO na jina hilo ni mji maarufu wa Japan.

Albamu hiyo itaachiwa rasmi Februari 16 mwaka huu na msanii huyo pia ameonyesha mchoro rasmi utakao tambulisha albamu hiyo kwa kuposti katika kurasa zake za Instagram na kuandika kwamba “This album is me opening my heart to you and I hope you enjoy it and love it as much as I do.”

MIGOS WATANGAZA WAZALISHAJI WA ALBAMU YAO CULTURE II

$
0
0


Quavo, Takeoff na Offset wa kikundi cha Migos wametangaza watu walioshiriki katika kuitengeneza Albamu yao iitwayo CULTURE II inayotarajiwa kuachiwa januari 26 mwaka huu.

 Kundi hilo la Atlanta wametumia kurasa zao za Instagram kutangaza watu hao. 


Kuna baadhi ya majina tulitarajia kabisa kuwa yatakuwepo kama Pharrell ambaye aliitengeza ngoma iitwayo ‘Stir Fry’ ambayo ni moja kati ya ngoma aliofanya na Migos lakini pia kuna majina ya wasanii wakubwa kama vile Kanye West, Murda Beats na Cardo. 
A post shared by Migos (@migos) on

DAWA ZA KULEVYA ZAZIDI KUMUWEKA CHID BENZ POLISI

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Chid Benz bado anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya.

Jeshi la polisi mkoani humo limesema bado linaendelea kumshikilia msanii huyo na baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani pamoja na washtakiwa wenzake.

Chid Benz alikamatwa December 30 mwaka jana, 2017 akiwa na mke wake na vijana wawili.

NEW VIDEO:- BURNA BOY - HEAVEN'S GATE (FEAT. LILY ALLEN)/SEKKLE DOWN (FEAT. J HUS)

$
0
0

Spaceship anchorman, Burna Boy kicks off the new year, 2018, right off from where he left it off in 2017 with a smoking new tune that he titles “Heaven’s Gate.” He features English singer, Lily Allen on this one.


Now for full disclosures, “Heaven’s Gate” holds nothing Afro in its grind and heat. In fact, Burna Boy whose real name is Damini Ogulu broke down the barriers of borders and boundaries on this latest fierce.


The thing is, the “Pree Mi” hitmaker simply delved into a myriad of styles, genres and patterns; sealing things off with his dancehall kinda flavour that simply stuns.


This is no surprising since Bunrna Boy has managed a world of releases dating back to the past year with such records as “Sekkle Down,” “Temper,” “Deja Vu,” Gba,” , Koni Baje.”.


Now, if you do not get the bigger picture that OluwaBurnais working towards a project with “Heaven’s Gate,” then we might actually not be living on the same planet.


Lily Allen whose real name is Lily Rose Beatrice Cooper comes through with the perfect ladders of support. She brought on her abilities as a multi-talented singer, songwriter, actress, and television presenter to bare on “Heaven’s Gate.” Well, we might not finish this review if we begin to list several of her hit records.


With a music video to match, you wouldn’t believe “Heaven’s Gate”is one screamer off the stables of Nigeria’s very own Burna Boyas it holds the touch of global excellence.


You’ve just got to delve right into this masterclass presentation for a banging weekend yet ahead. Simply stream, download, then share your thoughts and opinion in the comments section below.

NIPO TAYARI KUWAANDIKIA OFFSIDE TRICK NA LIPO JAMBO NALOJUTIA KUHUSU WAO:- AT

$
0
0


Kwa zaidi ya Miaka 7 kumekuwepo kwa Bifu kubwa ya maswahiba wa muda mrefu baina ya Wasanii wa Mduara baina ya Mfalme wa muziki huo AT na kundi la Offside Trick ambapo awali walikuwa wakifanya kazi pamoja.

AT ambae kwa sasa anafanya poa na ngoma yake iitwayo Kazi Yako, amekiri kujutia kuwajibu wasanii wa kundi la Offside Trick kupitia ngoma zake za Vifuu Tundu na Bao la kete kwa kuwa anahisi ndio chanzo cha kupotea kwao.

"Niseme ni kweli nilikuwa na Bifu na Offside Trick, aaah na mimi mwenyewe niseme kwamba yaani bora nisingewajibu, na ningeendelea kuimba kuliko kuwajibu kupotea kabisa kwa hiyo natamani uwepo wao wawepo lakini wafanye kazi zao kwaajili ya raia na sio kwaajili yangu mimi" amesema AT.

Pia AT amezungumzia mstakabali wa kufanya kazi na Offside Trick.

"Sijajua kama ipo siku nitafanya nao kazi kiukweli kwa sababu Offside Trick ambayo mi nimezinguana nayo sio hii iliyokuwepo kwa hiyo ni vitu vingine. Chochote kile kama raia wakiniruhusu huenda nikafanya nao kazi kwa sababu mashabiki wangu sitaki kuwa kera" amesema AT.

Hata hivyo AT ameongeza kwa kuzungumzia msaada ambao anaweza kuutoa kwa Offside Trick ili kurejea katika gemu.

"Kwa hiyo naweza kuwasaidia kuwaandikia lakini siwezi kuimba nao sauti ikawa pamoja na wao, lakini mashabiki wakisema hebu fanya kitu tuone mna-sound aje naweza kufanya nao ni washikaji ambao nimeweza kufanya nao kazi kwa muda mrefu" amesema AT.

MAJINA YA KIBANTU YANAONGEZA UKUBWA WA NGOMA KUPENYA BUSHOKE

$
0
0


Mwanamuziki mkongwe Ruta Maximilian Bushoke a.k.a Bushoke amekiri kutumia majina ya Kibantu katika nyimbo zake yamekuwa msaada mkubwa kwa muziki wake kupenya kitaani.

Bushoke ambaye kwa sasa anafanya vema kwenye gemu la muziki wa kizazi kimpya na ngoma iitwayo Goma la Ukae, iliyotayarishwa na Producer Abby Dady kutoka Square muziki ameiambia The Splash ya Ebony FM inayotangazwa na Chris Bee na Fredoo Mbunji namna anavyoabudu majina ya kibantu.

"Ukae ni nyumbani ni kibantu kuna baadhi ya makabila mawili matatu yanatumia kwa hiyo siwezi kusema ni kizaramo au nini kwa sababu sio specific ni kizaramo pekee ake au labda kabila fulani pekee yake bali ni kibantu kiujumla kwamba Goma la Ukae ni goma la nyumbani au linalochezwa nyumbani" amesema Bushoke.

Hata hivyo ameeleza sababu za msingi zakufanya kazi na Producer Abby Dady.

 "Nilivyomchunguza ni mtu ambae anapiga piga sana ngoma kati ya maproducer ambao wamejaaliwa sana kwenye upande wa ngoma, anavyotengeneza beat Abby Dady yupo vizuri kuja na kitu cha pekee yake kwa hiyo niliona kwa sababu Goma la Ukae ni kitu cha utofauti basi nimpatie Abby Dady" amesema Abby Dady

Tazama Video Mpya ya BUSHOKE - GOMA LA UKAE.

MSONGO WA MAWAZO HUSABABISHA UNENE?

$
0
0


Sote tunafahamu nini kinatufanya tunenepe: ulaji wa vyakula vyenye kalori kupita kiasi.

Japo jibu hili ni la kweli, halijibu swali la msingi zaidi - je, ni kwanini watu hula chakula kupita kiasi?

Ni kwa nini wakati mwengine najihisi kula keki ama chokleti licha ya kwamba nafahamu nitajutia baada ya dakika chache zijazo?

Kwa mara nyingi huwa ni tamaa - ama ni kitu chengine kinachoendelea?

Licha ya kwamba nidhamu ni muhimu, kuna ushaidi mwingi kwamba msongo wa mawazo huchangia pakubwa kwa mtu kuongeza kilo za mwili.

Msongo wa mawazo kupita kiasi, huathiri jinsi mtu anavyopata usingizi na viwango vya sukari mwilini. Hali hiyo huongeza njaa na kuzidisha zaidi ulaji wa chakula kwa utaratibu.

Na hali hiyo huathiri zaidi usingizi, hata viwango vikubwa vya msongo wa mawazo huathiri zaidi viwango vya sukari. Kwa muda, huo unaweza kusababisha viwango vikubwa vya mafuta na kisukari aina ya type -2.

Na kuona kile kinachoweza kutokea, Dkt Giles Yeo, mwanachama wa Trust Me ,yeye ndiye daktari wa timu ambayo pamoja na usaidizi wa wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Leeds, aliamua kujiweka yeye mwenyewe kwenye katika hali ngumu ya msongo wa mawazo.

Wanasayansi wa Leeds walianza kwa kumuuliza Giles kufanya mambo tofauti ambayo yangemsababishia msongo wa kiakili.

Walimuweka mbele ya tarakilishi na wakamlazimisha kufanya hesabu ya kuondoa ,17 , kutoka kwa nambari kama 2,043. Na alipokuwa akikosea, waliona akipatwa na hali ya msongo wa mawazo jambo ambalo lilimpatia Giles shida.

Baada ya hapo wakamlazimu kuweka mikono yake kwenye beseni ya maji baridi kwa muda. Kabla na baada ya uchunguzi huo, kikosi hicho cha chuo kikuu cha Leeds wakampima kiwango cha sukari.
Kiwango cha sukari mwilini huongezeka wakati mtu anapokula, na kwa mwenye afya njema kama Giles, kiwango hicho cha sukari hushuka na kuwa kawaida kwa haraka.

Lakini kikosi hicho cha Leeds kilibaini kwamba siku ambayo Giles alikuwa amepitishwa kwenye shida hizo zote, bado kiwango cha sukari kilichukua muda wa saa tatu kurudi katika hali ya kawaida ambayo ni mara sita zaidi katika siku ambayo mtu ametulia bila wasiwasi wowote. 

Sababu kuu ambayo husababisha hayo ni kwamba endapo mtu anapata msongo wa mawazo, mwili hujipata ''ukipigana.'' 

Mwili hudhani uko katika mashambulizi na hutoa glukosi kwenye damu ili kuongeza nguvu kwenye misuli.

Lakini endapo huhitaji nguvu za kukimbia kujiepusha na hatari yoyote ile, basi wengi hutoa insulini ili kuweza kurudisha kiwango cha sukari kwa kiwango cha kawaida.

Ongezeko la kiwango cha insulini na kushukwa kwa kiwango cha sukari humfanya binadamu kuhisi njaa na ndio sababu kuu kumfanya mtu kutamani kula vyakula vya sukari hasa iwapo mtu anakumbana na msongo wa mawazo.

Kitu kama hicho hutokea iwapo hujapata usingizi mzuri usiku. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na watafiti wa chuo kikuu cha King, mjini London imebaini kwamba iwapo mtu akikosa usingizi anauwezo wa kula zaidi ya kalori 385 kwa siku , ambayo ni sawa na kalori iliyoko kwenye keki ndogo. 

Watoto pia hupata tamaa ya vyakula vya sukari iwapo hawajalala vizuri, kwenye utafiti mwengine,wa hivi karibuni, watafiti walichukua kikundi kidogo cha watoto wenye umri wa miaka mitatu na minne ambao hulala kila siku mchana na kuwalazimu kutolala mchana mmoja na kuhakikisha wamekaa macho saa mbili zaidi wakati wao wa kwenda kulala kila siku. 

 Siku ya pili ,watoto hao walibugia asilimia 20 ya kalori kuliko kawaida, hasa vyakula vyenye sukari nyingi na waliruhisiwa kulala kwa muda waliotaka.

Na siku ya tatu, bado watoto hao walikula kalori asilimia 14 kuliko kawaida.

Jinsi za kupunguza msongo wa mawazo kila siku?
Kitu cha kwanza, ningependa watu wanashauriwa kupata usingizi wa kutosha. Hili ni rahisi kwa kusema na si kwa vitendo, lakini mamlaka ya huduma ya afya-NHS inatupatia mbinu muhimu za kufuata.

Pia ungejaribu njia ambazo zinazofahamika zinazopunguza msongo wa mawazo kama vile mazoezi, ukulima ama kushiriki mazoezi ya yoga.

Lakini kitu muhimu tulichobaini kwenye utafiti wetu ni kwamba utafaidika iwapo ulifurahia.
Kwa hivyo jaribu kufanya vitu tofauti na uone kile kinachoweza kukufaa.

TETESI MBALIMBALI ZA USAJILI WA WACHEZAJI NA SOKA 25 JANUARI 2018

$
0
0


Manchester City huenda ikaingia katika makubaliano na Atletico Madrid kubadilishana mshambuliaji raia wa Argentina Sergio Aguero, mwenye umri wa 29, kwa upande wake imchukue Antoine Griezmann, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 katika msimu ujao wa joto. (Sun)

Lokomotiv Moscow imeifuata Liverpool kumtaka kumsajili winga mwenye umri wa miaka 23 Lazar Markovic. Msimu uliopita Mserbia huyo alichukuliwa kwa mkopo huko Sporting Lisbon na Hull City. (Mirror)

Chelsea imekubaliwa ombi lenye thamani ya pauni milioni 44, na marupurupu kwa mshambuliaji wa Roma Edin Dzeko, na full beki raia wa Brazil Emerson Palmieri. (Guardian)

Kipa raia wa Uhispania wa Getafe Vicente Guaita, mwenye umri wa miaka 31, amefuzu uvipimo vya kiafya huko Crystal Palace - lakini mazungumzo yangali yanaendelea kuhusu iwapo atajiunga na timu hiyo sasa au katika msimu wa joto. (Mail)

Brighton imewasilisha ombi la pauni milioni 6 kwa mlinzi wa Bristol City Aden Flint, aliyedhihirisha umahiri wake katika mashindano ya taji la Carabao. (Argus)

Klabu ya Ufaransa Monaco imekubali kumuuza mshambuliaji raia wa Argentina Guido Carrillo, kwa Southampton kwa pauni milioni 19.2. (Telegraph)

Sevilla imekubali makubaliano ya kumsajili mchezaji kiungo cha kati wa Swansea City Roque Mesa, mwenye umri wa miaka 28, kwa mkopo kwa muda uliosalia. (Marca - in Spanish)
 
West Ham inatarajiwa kumsajili raia wa Ureno Joao Mario, mwenye umri wa miaka 25, kutoka timu ya Inter Milan. Makubaliano ya awali yamefikiwa baina ya mchezaji huo na klabu hiyo ya Italia.

Meneja wa Barcelona Ernesto Valverde anasema klabu hiyo ya Uhispania haitosajili walinzi wengine wowote licha ya kuondoka kwa Javier Mascherano, 33, kuelekea katika ligi kuu ya Uchina timu ya Hebei Fortune. (ESPN)

 Aston Villa inakaribia kumaliza makubaliano ya kumchukua kwa mkopo beki wa kati wa timu ya Manchester United Axel Tuanzebe. (Express)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Sunderland Jack Rodwell,anafanyiwa majaribio katika timu ya Vitesse Arnhem. (Chronicle)

Mshambuliaji wa Ipswich Town David McGoldrick, mwenye umri wa miaka 30, anaonekana kulengwa tena na Cardiff City. (Wales Online)

Wachezaji wa West Brom James Morrison, na Chris Brunt, wameanza kuandaa taarifa ya pamoja kwa msimu ujao wa joto. (Express & Star)

Mchezaji mpya wa Manchester United Alexis Sanchez aikagua nyumba ya vyumba vitano vyenye thamani ya £2m - iliyo na chumba maalum kilicho na kinanda. (Mail)

Club America ya Mexico itamuekea vikwazo Carlos Darwin Quintero baada ya mchezaji huyo wa kiungo cha mbele mwenye umri wa miaka 30 kumpiga mpira mwandishi habari wakati wa matangazo ya moja kwa moja. (Goal)

WASANII WAKONGWE HATUSHINDWI KUBUNI:- INSPECTOR HAROUN

$
0
0

Rapper INSPECTOR HAROUN amedai Wasanii wakongwe hawashindwi kubuni mbinu mpya za kiushindani katika muziki na badala yake wanafanya muziki unaoishi hali inayowafanya washindwe kuwa na utaratibu wa kuachia ngoma mara kwa mara.



"Ukiwa kimya mashabiki wanahisi umeishiwa, sisi hatutaki kutengeneza muziki wa Big G, sisi tunatengeneza muziki unaoishi hatutengenezi muziki wetu kwa siku moja au mwezi mmoja au kila baada ya nusu mwezi kuachia ngoma. Muziki unaoishi unatakiwa uutengeneze ndani ya miezi kadhaa halafu maproducer tofauti tofauti wanakaa na kufanya kitu kizuri". amesema Inspector Haroun.



Akiendelea na utetezi wa kauli yake Hitmaker huyo wa Pamba Nyepesi Inspector Haroun amesema "Kuna kitu ambacho mashabiki wa muziki kwa sasa wanakimiss, sawa wadogo zetu wanafanya vizuri, wanaimba vizuri wapo wengi wananyakua Tuzo na wengine wanaishia kuwa nominated lakini hawana uhalisia ukimsikia msanii huyu anafanana na msanii fulani unashindwa kuwatofautisha".



Inspector Haroun anatoa ushauri upi kwa wasanii wa sasa? "Kikubwa wasanii walioingia katika gemu ni kuzingatia identity yao, uwepo wao wautambue unatakiwa kuwa kama wewe, wakati unapoanza muziki lazima utadokoadokoa sehemu ili upate njia yako ukishapata unatengeneza mfumo ya kujulikana kama wewe ndio maana sasa hivi AY, Juma Nature, Prof J, Afande Sele, Jay Moe na wengineo wanajulikana kama wao".


Viewing all 911 articles
Browse latest View live