Quantcast
Channel: CHIMBUKO LETU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 911

UEFA YAFANYA MABADILIKO KATIKA MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA

$
0
0


Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limefanya baadhi ya mabadiliko katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya na Europa League, mabadiliko hayo yataanza msimu ujao 2018/19. 
 
Timu zitaruhusiwa kufanya mabadiliko (Sub) ya nne endapo mechi itaenda "Extra Time" katika hatua ya mtoano. 
 
Mara zote katika mechi za michuano hiyo, ni wachezaji 18 huandikwa katika karatasi ya mechi, 11 wanaanza huku 7 wakiwa benchi, kuanzia msimu ujao itakuwa ni hivyo hivyo katika mechi zote kasoro mechi za Fainali Klabu Bingwa Ulaya, Fainali Europa League na UEFA Super Cup, ambapo katika mechi hizo karatasi ya mechi itajumuisha wachezaji 23, 11 wanaanza huku 12 wakiwa benchi. 

Hii itawapa makocha uwanja mpana wa kuchagua wachezaji katika mechi hizo muhimu. 
 
Mabadiliko mengine ni katika usajili, timu zitaruhusiwa kusajili wachezaji wapya watatu baada ya mechi za makundi bila ya vizuizi vyovyote, hivyo makocha watapata uhuru zaidi katika sajili zao katika dirisha la januari.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 911

Trending Articles