Mmiliki wa Albamu ya "Money Modays"Vanessa Mdee, afunguka siri ya mafanikio yake yametokana na Hayati Whitney Houston kwa kuwa familia yake ilikamilisha ndoto za kuonana na aliyewahi kuwa mwanamuziki nguli huyo ulimwenguni.
Kufuatia kukutana kwake kulichagiza Vanessa Mdee kukitia chachandu kipaji chake cha uimbaji nakujikuta akifuata nyayo za mkali huyo wa kibao cha "I Will Always Love You".
"Nilitambulishwa kwa Whitney Houston nikiwa mdogo sana kupitia wazazi wangu, kwa hiyo nyumbani kwetu tulikuwa tunacheza sana nyimbo za Whitney Houston, Steve Wonder na Michael Jackson" amesema Vanessa Mdee.
Hata hivyo Vanessa Mdee amefungukia namna alivyokuwa akikoshwa na sauti ya Hayati Whitney Houston.
"Unajua kwanza kama Vocalist mi ni mtu ambaye anani-inspire hata context ya miziki yake huwezi kujua kama alikuwa anaimba Gospel naona nyimbo zake ni gospel ni kitu ambacho nampendea aliweza ku-crossover na ku-trend kwa kufanya muziki waku-inspire nakuhamasisha bila ku segregate waislamu na wakristo" amesema Vanessa Mdee.