Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania TOP C katika pozi
Mkali wa Lofa TOP C ambaye ni miongoni mwa wasanii waliopo chini ya management ya Candy n Candy Records ya nchini
Akifunguka kupitia Kipengele cha Bomba Base Show kinachorushwa kupitia Bomba Fm Radio kilichopo Mbeya Top C amesema “Mikakati yetu na ile kampuni bado haijakuwa katika mstari ambao unaeleweka kuna vitu vingi sana ambavyo kampuni imeahidi lakini bado havijaanza kutendeka kazi unaonena vile kama kuna ubabaishaji mwingi”.
“Kikubwa ambacho nakifanya kwa sasa, kuna harakati fulani ambazo zinafanyika nadhani ikiwa watu wameshaupitia mpaka Jumatano hivi, tunaweza tukawa tumejua nini tunakifanya ili kuvunja ule mkataba” aliongeza TOP C kuna watu wakiwa .
Je, haoni kama kuvunja mkataba kunaweza kukuathiri katika soko la muziki na kubaki katika msoto ? TOP C anajibu kuwa “ Hauwezi kuniathiri kwa sababu mkataba unavozungumza unakuwa na muda wa kufanya promotion na muda fulani mtakuwa mmefanya nyimbo ngapi, ukiona vitu hivyo havitekelezeki unaweza tu kuomba kunatokana na vitu hivi na hivi vinashindikana, unajua unavyosaini mkataba lazima ujue kunamisingi ya kuvunjika pia sio ukipata matatizo wewe uendelee kuvuimilia humo humo lazima usaini mkataba ambao ukiona vitu Fulani mlivyokubaliana havitendeki uwe na uwezo wa kuuvunja”.