Baada ya come back yake kwenye Bongo Flava na Ngoma ya Goma La Ukae Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania Ruta Maxmilian a.k.a Bushoke anatarajia kudropisha albamu yake mpya.
Bushoke amesikika na exclusive hiyo kwenye The Splash ya Redio Ebony FM wakati akipiga stori na Watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji.
“Kiukweli kabisa kuna nyimbo nimefanya na Nandy, Maua na wasanii wengine tofauti tofauti kwa hiyo hii ni project ya Albamu kwa hiyo napenda watu wasubiri albamu yangu, pia miaka ya nyuma nilikuwa naachia wimbo na kutulia naachia nyimbo nakutulia(msisitizo) hata sasa hivi siwezi sema nitakuwa naachia nyimbo tap tap tap sema kwa kuwa nimekaa kimya sana kweli nitatoa nyimbo baada ya nyimbo” amesema Bushoke.
Bushoke anaendelea na ufafanuzi wa nini kitafuata baada ya kuachia albamu yake ambayo itakuwa imesheheni madini yakutosha.
“Lakini baada ya kuachia albamu sito harakisha tena kuachia nyimbo nitaacha watu wasikilize albamu then naendelea na nyimbo nyingine kama kawaida kuna nyimbo kibao sio Goma La Ukae pekee ake, kuna nyimbo inaitwa Chechu, Tupendane Sasa kuna nyimbo nyingi sana kwa hiyo mashabiki wasikilizie tu” amesefunguka Bushoke.